Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Yuda alitoka katika mwaliko huo kufanya njama ya kumsaliti Yesu

  Lakini mtazamo wa Yesu aliomtazama Yuda ulimdhihirishia kuwa, Yesu alisoma unafiki wake wa kujifanya kuwa mfuasi wa Yesu, huku ni mlaghai tu. Na katika kumsifia Mariamu Kristo alimkemea Yuda. Kemeo hilo lilimwumiza Yuda, naye akatoka na kumwendea kuhani mkuu, ili kumsaliti Yesu.TVV 314.3

  Viongozi wa Israeli walikuwa wamepata fursa ya kumpokea Kristo kama Mwokozi wao, bila fedha na bila gharama. Lakini waliikataa karama yenye thamani na wakamununua Bwana wao kwa vipande thelathini vya fedha.TVV 314.4

  Yuda alionea husuda tuzo la Mariamu la marhamu ya thamani kwa Yesu. Moyo wake uliwaka kwa wivu vipi Mwokozi asitahili kupokea tuzo waliyostahili wafalme wa dunia. Kwa gharama pungufu kuliko thamani ya marhamu, alimsaliti Bwana wake.TVV 314.5

  Wanafunzi hawakuwa kama Yuda. Wao walimpenda Mwokozi, ila hawakuifafanua kwa dhati tabia yake. Mamajusi kutoka Mashariki ambao walijua mambo machache sana kuhusu Yesu, walionyesha kutambua kwa dhati heshima iliyompasa.TVV 314.6

  Kristo huthamini vitendo vya ustahifu utokao moyoni. Hakulikataa ua la kawaida lililochumwa na kutolewa na mkono wa mtoto kwa upendo. Alizikubali sadaka za watoto, na kuwabariki watoaji. Katika Maandiko, kwa Mariamu kumpaka Yesu marhamu hutajwa katika kumtofautisha na Mariamu wengine. Matendo ya upendo na taadhima ni ushahidi wa imani katika Yesu kama Mwana wa Mungu.TVV 315.1

  Kristo aliukubali utajiri wa upendo safi wa Mariamu ambao wanafunzi wake hawakuweza, wasingeweza kuuelewa. Ulikuwa upendo wa Kristo uliomshurutisha. Yale marhamu yalikuwa mfano wa moyo wa mtoaji, uthibitisho wa nje wa upendo uliojazwa na vijito vya mbinguni hadi ukafururika. Upweke wa Kristo, kuishi kwake maisha ya kibinadamu, kamwe hayakufurahiwa na wanafunzi kama ilivyopaswa kuwa. Mara nyingi alihuzunishwa. Alifahamu kuwa ikiwa wangekuwa chini ya mvuto wa malaika wa mbinguni waliofuatana naye, na wao pia wasingefikiria sadaka yo yote ile kama yenye thamani tosha kuutangaza upendo wa moyoni.TVV 315.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents