Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Herode afanya Mauaji ya kutisha

    Herode alingojea kurudi kwa mamajusi, akiwa Yerusalemu Muda ulipopita bila kupata lolote, tuhuma yake ilizidi. Je, walimu wa Kiyahudi wamemfunulia mipango yake au mamajusi wameulaghai? Aliwaza akachanganyikiwa. Akaazimu kuchukua hatua ya nguvu.TVV 31.5

    Maaskari walitumwa kwenda Bethlehemu kuwaua watoto wote wenye miaka miwili na kurudi chini. Nyumba za mji wa Daud;l uliokaa kitulivu kwa miaka 600 kabla haujafunguliwa kwa nabii, ulishuhudia maovu hayo. Unabii ulisema kuwa, “katika Rama zilisikika sauti za kilio na maombolezo makuu. Raheli akiwalilia watoto wake, asikubali kufarijiwa, maana hawapo.”TVV 31.6

    Ajali hii Wayahudi walijiletea wenyewe. Wamemkataa Roho Mtakatifu, ambaye ndiye ngao yao. Wamechunguza unabii na kuutafsiri kama wapendavyo wenyewe, kwamba wao wanapendelewa, na mataifa mengine la. Wamechochea chuki ya mtawala wao. Kwa njia ya kumweleza Kristo kimakosa na kazi yake pia, Shetanii. aliazimu kumharibu Mwokozi, lakini badala yake maafa yamewageukia wenyewe.TVV 31.7

    Mara baada ya kuwaangamiza watoto, Herode alikufa kifo kibaya sana. Yusufu bado yuko Misri. Malaika akamwagiza arudi katika Israeli. Kuhusu Yesu, ambaye ni mirithi wa kiti cha enzi cha Daudi Yusufu alitamani kuishi Bethlehemu. Lakini alipojua kuwa Arklao mtoto wa Herode anatawala badala ya baba yake, aliogopa asije akafanya yale yale ya baba yake. Yusufu alionyeshwa mahali pa salama zaidi, Nazareti. Hapa ndio Yesu alipokulia kwa muda wa miaka karibu thelathini, ili neno litimie kuwa: “Ataitwa Mnazerayo.” Galilaya kulikuwa na mchanganyiko wa mataifa kuliko Uyahudi. Kwa hiyo Wayahudi hawakupashughulikia.TVV 32.1

    Hivyo ndivyo Mwokozi alivyopokelewa, alipokuwa ulimwenguni. Mungu hakumwaminisha Mwanawe mpendwa kwa binadamu, hata alipokuwa akiwashughulikia kuhusu wokovu wao. Aliwaamuru malaika kumhudumia Yesu, mpaka atimize kazi yake, na kufa mikononi mwa wale aliokuja kuwaokoa.TVV 32.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents