Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kristo alikatisha tamaa tumaini la ukuu wa duniani

    Katika mahubiri mlimani Kristo alitaka kufuta kazi iliyofanywa na walimu wa uongo, na kuonyesha ukweli wa ufalme wake. Bila kueleza jinsi ufalme wa mbinguni ulivyo, hakuwaambia wasikilizaji wake masharti ya kuuingia, akiwaacha wafikiri wenyewe jinsi ufalme huo ulivyo. Alisema: “Wa heri wanaofahamu umaskini wao wa kiroho, na wanatafuta kuponywa katika hali hiyo.” Injili haisemi juu ya kiburi cha kiroho, bali kwa wanyenyekevu, wenye roho iliyopondeka.TVV 162.1

    Wenye moyo wa kiburi hushindana kuingia katika ufalme kwa nguvu na kwa matendo yao, lakini haki yetu na kufaa kwetu kuingia mbinguni hutokana na haki ya Kristo. Bwana hawezi kumfanyia mtu kitu cha kumsaidia, mpaka amejitolea kamili kwa Mungu, na kutawaliwa naye kamili. Ndipo anaweza kupokea kipawa ambacho Mungu huwapa watu. Mtu anayejisikia kuwa na haja, hatanyimwa chochote. Angalia Isaya 57:15.TVV 162.2

    “Wa heri wenye huzuni: maana watafarijika.” Huzuni anayozungumzia sio ile ya kuhuzunikia jambo lililotukia kwa mtu, na kumfanya aomboleze. Mara nyingi sisi huhuzunika kwa ajili ya matokeo ya matendo maovu tuliyotenda. Lakini huzuni ya kweli huja kwa njia ya kazi ya Roho Mtakatifu afanyaye kazi ndani yetu, na kutudhihirishia ubaya wa dhambi hasa. Roho Mtakatifu hutufikisha chini ya msalaba. Hapo huona kuwa kila dhambi tutendayo humsulibisha Yesu kwa upya. Tunapomwangalia akiteseka msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, huhuzunika na kuacha kufuata njia za dhambi hizo. Huzuni hii humfunga mwenye huzuni na Mungu. Na machozi ya mwenye huzuni huwa kama matone ya mvua yanayotangulia nuru ya jua kuleta utakatifu. Na huo hutangaza furaha ya kudumu, itakayokuwa kama chemchemi katika moyo wa mtu. tazama Yeremia 3:12, 13; Isaya 61:3.TVV 162.3

    Wale wanaohuzunika kwa njia hiyo watafarijika. Kwa njia ya mateso na dhiki Mungu hutufunulia madahra yaliyomo katika tabia zetu, ambazo zapaswa kushindwa kwa neema yake. Mambo mabaya yaliyo katika tabia zetu, ambayo hatuyafahamu, Mungu hutufunulia. Na hapo sisi hupata mtihani kama tutafuata njia ya Mungu, au tutang’ang’ania tabia zetu ambazo ni za madhara. Tupatapo jaribu tusipoasi au kunung’unika tukiwa mikononi mwa Yesu, tutapita. Njia ya Mungu machoni mwa wanadamu huonekana kuwa giza, na isiyokuwa ya kupendeza. Lakini njia hiyo ndiyo ya huruma, na mayokwenda wokovuni.TVV 162.4

    Neno la Mungu kwa wenye huzuni ni: “Nitageuza huzuni zao kuwa furaha, nami nitawafariji.” Yeremia 31:13.TVV 163.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents