Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    54 — Msamaria Mwema

    Wakati Kristo alipokuwa akifundisha watu, Mwanasheria mmoja alisimama, akamjaribu na kusema: “Bwana nitafanya nini ili niurithi uzima wa milele?” Makuhani na Marabi walikuwa wakitaka kumtatanisha Kristo, kwa kutaka Mwanasheria, amwuliza swali la namna hiyo. Lakini Mwokozi hakutaka mabishano. Kwa hiyo alisema: “Kumeandikwa nini katika sheria? Unasomaje humo?’ Aliligeuza swali hilo la wokovu kuwa mambo yahusuyo amri za Mungu.TVV 281.1

    Mwanasheria akasema: “Mpende Bwana Mungu kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa nia yako yote, na jirani yako kama nafsi yako.” Yesu akasema: “Umesema vema, enenda ukafanye hivyo ndipo utaishi ”TVV 281.2

    Mwanasheria alikuwa akijifunza maandiko mtakatifu apate kujua maana yake. Katika jibu lake kuhusu matakwa ya sheria, alisema kuwa hakuna faida ya kukariri-kariri tu maandiko ya sheria bila vitendo. Lakini kuna matendo mawili hasa ambayo hutegemewa na sheria yote na manabii pia. Jibu lililosifiwa na Kristo lilifanya Marabi na Mwokozi wakabiliane uso kwa uso.TVV 281.3

    Yesu aliposema “Fanya hivyo, ndipo utaishi”, aliiweka sheria katika mwungano wa Mungu. Haiwezekani kushika sheria moja na kuvunja nyingine. Kanuni ile ile huhusu zote, yaani kumpenda Mungu na mwanadamu; ndivyo vitakiwavyo katika maisha.TVV 281.4

    Mwanasheria alikubaliana na usemi wa Kristo. Hakuwa akionyesha upendo kwa wenzake. Lakini badala ya kutubu, alijaribu kujitakasa kwa kusema: “Jirani yangu ni nani?” Katika Wayahudi swali hili lilikuwa na msukosuko. Watu wa mataifa na Wasamaria walihesabiwa kama wageni, na maadui, lakini ni wapi ubaguzi wa makabila na utengano wa watu unapotoka? Je, watawahesabu wajinga na watu duni katika jamii moja kuwa ‘wachafu’ nao ni jirani pia?”TVV 281.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents