Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mwenye imani Haba

  Filipo alikuwa mtu wa kwanza aliyepewa agizo na Yesu kusema, “Nifuate.” Alikuwa amesikia Yohana akimtaja Yesu kuwa ni Mwana Kondoo wa Mungu. Alikuwa mtafuta ukweli hasa; ila alikuwa mwenye imani haba, kama imani yake ilivyoonyesha wakati alipomwita Nathanaeli. Ijapokuwa Kristo alitangazwa kwa sauti iliyotoka mbinguni kuwa ni Mwana wa Mungu, lakini kwa Filipo alikuwa “Yesu mwana wa Yusufu mtu wa Nazareti.” Yohana 1:45. Tena wakati watu 5,000 walipolishwa, Filipo alionyesha imani haba. Swali Yesu alilomwuliza kwamba,TVV 159.2

  “. . . Tununue mikate wapi, ili kuwalisha watu hawa ... ?” Lilikuwa la kumjaribu. Jibu la Filipo la kuonyesha imani haba, lilimsikitisha Kristo. Filipo alisema, “Mikate ya dinari mia mbili haitoshi kila mtu apate kidogo tu.” Yohana 6:5, 7. Filipo alikuwa amemwona Yesu akifanya kazi, na kuona uwezo wake, walakini hakuwa na imani.TVV 159.3

  Wakati Wayunani walipomwuliza Filipo kuhusu Yesu, hakujishughulisha kuwaonyesha Mwokozi na kueleza habari zake kwao, ila alikwenda kumweleza Andrea. Tena wakati ule kabla ya kusulibishwa kwa Yesu maneno ya Filipo yalionyesha imani haba. Wakati Toma aliposema, “Bwana ... tutajuaje njia?” Mwokozi alijibu, “Mimi ndimi njia .... Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu pia.” Filipo alisema maneno yenye imani haba, kwamba “Bwana tuonyeshe Baba, yatutosha.” Yohana 14:5-8.TVV 159.4

  Kinyume cha imani haba ya Filipo kulikuwa na imani kamili ya Nathanaeli. Nathanaeli alikuwa na imani ya kweli, siyo ya kuona kwanza mambo, bali imani kwa mambo yasiyoonekana. Walakini Filipo alikuwa mwanafunzi katika shule ya Kristo, na Mwalimu ambaye ni wa mbinguni alivumiliana na kutoamini kwa Filipo. Roho Mtakatifu alipomwagwa kwa wanafunzi Filipo alifundisha kwa hakika kabisa kiasi cha kutubisha watu wasioamnini; ambao walimsikiliza.TVV 159.5

  Yesu alipokuwa akiwatayarisha wanafunzi ili wawekewe mikono ya uchungaji, mmoja ambaye hakuitwa alidai ili awe mmoja wao pia. Yuda Iskariote aliyejidai kuwa mmoja wa wafuasi wa Yesu, alikuja ili awe mmoja wao wa hawa wanaotayarishwa kuwekwa mikono. Kwa kujiunga na wanafunzi alikuwa akitamani kupata madaraka makubwa katika ufalme huo mpya. Alikuwa mtu mtaalamu sana, mwenye uwezo na akili sana. Wanafunzi walimshuhudia kwa Yesu, na kumtaka amkubali kuwa mwenzao, ambaye atamsaidia sana kazini. Kama Yesu angalimkataa Yuda wanafunzi wangalikuwa na mashaka juu ya Yesu. Walakini hali ya Yuda ingeonyesha hatari katika kazi ya Mungu, maana ingeleta kanuni za kidunia ambazo hazitakiwi katika kazi ya Mungu.TVV 160.1

  Walakini Yuda alijisikia kuwa katika hali ya kuongoa roho za watu kwa Mwokozi. Yesu asingalimkataa mtu huyu aliyejiingiza kuongoa roho. Mwokozi alisoma moyo wa Yuda; aliona uovu umo ndani yake, kama hatasaidiwa na Mungu, atazama. Katika kuunganika na mtu huyu, Yesu alimweka mahali panapofaa, siku kwa siku alimshirikisha na huduma yake isiyokuwa ya ubinafsi. Kama Yuda angefungua moyo wake kwa Kristo, angaliweza kuwa raia wa mbinguni.TVV 160.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents