Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  47 — Kupingana na Roho za Mashetani

  Jua lilipochomoza Yesu na wanafunzi wake, walitelemka kutoka mlimani. Wanafunzi walikuwa kimya kwa ajili ya maajabu waliyoona. Wangalikaa mahali hapo patakatifu kwa furaha, lakini kulikuwa na kazi iliyowapasa kufanya.TVV 242.1

  Chini ya mlima kulikuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu. Mwokozi alipowasogelea, aliwaagiza wale wanafunzi watatu kuwa wasimwambie mtu kuhusu mambo waliyoona. Alisema, “Msimwambie mtu habari ya njozi hii, mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu.” Kusimulia njozi hii kwa watu kungaliwashangaza tu, bila kitu cha zaidi. Walielewa kiasi gani hata kwa wale watatu, kwamba kufufuka katika wafu maana yake ni nini. Walakini hawakumwuliza Yesu awafafanulie zaidi.TVV 242.2

  Watu waliokuwa uwandani walipomwona Yesu akija, walimkimbilia ili kumsalimu walakini alipoangaza macho yake, alitambua kuwa kuna jambo lililotukia hapo, ambalo liliwakatisha tamaa wanafunzi. Baba mmoja alikuwa amemleta mwanawe ambaye alikuwa akisumbuliwa na pepo wachafu ili apate kuponywa. Yesu alikuwa amewapa wanafunzi uwezo wa kufukuza pepo na kuponya magonjwa, alipowatuma kwenda kuhubiri injili huko Galilaya. Walipokwenda kwa imani, mapepo waliwatii na kufukuzwa kutoka kwa watu. Sasa wanafunzi walisema kwa jina la Yesu kwamba pepo watoke kwa kijana huyu, lakini pepo waliwadhihaki tu wala hawakutoka. Wanafunzi bila kuona sababu ya kushindwa kwao, walijisikia kuaibika tu na kumwaibisha Bwana wao. Katika mkutano huo walikuwapo waandishi waliokuwa wakisema kuwa wamethibitisha kwamba wanafunzi na Bwana wao ni wadanganyifu. Hapo yuko pepo mchafu asiyeweza kushindwa na wanafunzi wala Bwana wao! Kundi lote liliona kuwa kushindwa kwao kumeleta aibu kubwa.TVV 242.3

  Lakini ghafla Yesu na wanafunzi wake watatu walionekana wakija. Kushirikiana walikoshiriki pamoja na wajumbe wa mbinguni usiku uliopita, kuliwaachia utukufu katika nyuso zao, kulikofanya nyuso zing’ae kwa watazamaji. Mwokozi alifika katika mkutano wenye ghasia. Akiwatazama waandishi, aliuliza, akisema, “Mnajadiliana kitu gani?” Lakini sauti zilizokuwa kali, zilizojaa ubishi zilinyamaa kimya. Sasa baba mwenye shida akanyosha njia kumwelekea Yesu. Akianguka miguuni mwa Yesu alisimulia hadithi yake ya shida ya mwanawe, akasema, ‘Bwana, nimemleta mwanangu kwako, ambaye ana pepo, na kumrarua . . . nilimleta kwa wanafunzi wako wasiweze kumponya.”TVV 243.1

  Yesu akaona hali ya kutokuamini mioyoni mwao, akasema, “Enyi kizazi kisichoamini, nichukuliane nanyi mpaka lini? Kisha akamwambia baba mwenye mtoto mgonjwa, ‘Mlete hapa mtoto wako.”TVV 243.2

  Mtoto aliletwa, na roho mchafu alimtupa chini. Akifurukuta kwa maumivu, alilala na kugaagaa na kukoroma.TVV 243.3

  Mara tena Mkuu wa uzima na mkuu wa giza walikutana Katika vita. Kristo, kutangaza kufunguliwa kwa wafungwa, kuwaweka huru waliojeruhiwa (Luka 4:18). Shetani, kutaka kuwashikilia wafungwa wake. Kwa muda kidogo Kristo aliruhusu pepo mchafu kuonyesha nguvu zake.TVV 243.4

  Yesu aliuliza, “Kijana huyu amesumbuliwa na pepo huyu kwa muda gani?’ Baba wa kijana alieleza muda mrefu wa mateso ya kijana. Kisha asipoweza kuvumilia zaidi, alisema, “Ukiweza fanya kitu. Tuhurumie utusaidie.” “Ukiweza” Mpaka sasa baba huyu angali akitia shaka kuhusu uweza wa Yesu. Kristo alijibu akasema, “Mambo yote huwezekana kwake aaminiye.” Baba akajibwaga miguuni pa Yesu, huku akiona hali yake ya kutokuamini, huku akilia na kusema, “Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu.”TVV 243.5

  Yesu akamgeukia mgonjwa akasema, “Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala, usimwingie tena.” Kukawa kilio cha maumivu, na mashindano makuu. Halafu kijana akalala kama mfu. Kukawa na mnong’ono katika mkutano wakisema, ‘Amekufa”. Lakini Yesu alimshika mkono, akamwinua, akamweka kwa baba yake mzima. Baba na mwanawe wakamsifu Mwokozi wao, wakati huo waandishi wameaibika, na kuondoka.TVV 243.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents