Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mwizi Mmoja Aliyesulibiwa Aamini

    Faraja moja ilimpata Yesu akiwa msalabani, nayo ilikuwa ombi la mwizi aliyetubu. Wezi wote wawili waliosulibishwa na Yesu, mara ya kwanza walimshu-. tumu; mmoja katika maumivu yake alizidi kukata tamaa na kuwa mkaidi. Lakini mwenzake hakuwa mhalifu mkaidi; hakuwa na hatia kama wengi waliokuwako pale msalabani. Mtu huyu alikuwa amemwona na kumsikia Yesu, lakini makuhani na wakuu walikuwa wamemzuia asimwamini. Katika ukaidi wake, mwisho alitumbukia katika makosa akakamatwa na kuhukumiwa.TVV 424.3

    Pale msalabani aliwaona waongozi wa dini wakimdhihaki Kristo. Alisikia hotuba ya dhihaka ikiungwa mkono na mhalifu mwenzake “Je! wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi.” Miongoni mwa wapita njia aliwasikia watu wengi wakirudia maneno ya Yesu na kusimulia miujiza aliyotenda. Mawazo, yakamrudia kuwa huyu ndiye Kristo. Akimgeukia mhalifu mwenzake akasema; “Wewe humwogopi hata Mungu nawe u katika hukumu hiyo hiyo”. Wale wezi waliokuwa wanakufa hawakuwa na cha kuogopa kutoka kwa mwanadamu. Lakini kwa mmoja lilikuja wazo dhati, kwamba kuna Mungu wa kuogopa, na kisha ya kumfanya atishike. Na sasa historia ya maisha yake ilikuwa karibu kufungwa. “Kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu? Nayo ni haki kwetu sisi; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa?”TVV 424.4

    Wakati yule mwizi alipohukumiwa kwa kosa lake alikata tamaa, lakini sasa kwa taratibu wazo la ajabu likamjia. Roho Mtakatifu akaangaza moyo wake na pole pole mnyororo wa ushahidi ukajiunga pamoja. Katika Yesu aliyedhihakiwa na kuangikwa msalabani, aliona Mwana kondoo wa Mungu. Tumaini likachanganyikana na huzuni katika sauti yake huku roho iliyokuwa inakufa ikijitupa kwa Mwokozi. “Ee Yesu, nikumbuke utakapokuja katika ufalme wako.”TVV 424.5

    Mara moja jibu likatoka, sauti ya upole yenye sauti ya wimbo, iliyojaa upendo na uwezo maneno: “Amini, nakuambia leo hivi, utakuwa pamoja nami peponi.” Luka 23:43. Yesu alikuwa amengoja kwa hamu kusikia maneno ya faraja kutoka kwa wanafunzi wake. Alikuwa amesikia maombolezo tu, “Tulitumaini kwamba huyu ndiye ambaye angekomboa Israeli.” Maneno ya imani na upendo kutoka kwa mwizi anaye kufa msalabani yalileta faraja kuu kiasi gani kwa Mwokozi! Wakati ambapo hata wanafunzi walikuwa na mashaka, maskini mwizi alimwita Yesu “Bwana.” Hakuna aliyemkiri akiwa msalabani isipokuwa mwizi mwenye toba aliyeokolewa saa ya mwisho kabisa. Sauti ya huyu mtu mwenye kutubu, iliwasitua waliosimama kando kando. Wale waliokuwa wakigombea mavazi ya Kristo waliakoma ubishi wao wakangojea jibu kutoka katika mdomo wa Kristo anayekufa. Aliposema maneno ya hadi giza lililokuwa limeufunika msalaba lilichomwa na mwanga hai. Kristo katika hali yake ya kudhalalishwa alitukuzwa. Yule ambaye aliyeonekana machoni pa wote kuwa ameshindwa alikuwa Mshindi. Alitambulika kuwa Mchukua Dhambi. Wanaweza kugawana nguo zake, lakini wasingaliweza kunyakua uwezo wake wa kusamehe dhambi. Ni haki yake ya kifalme kuwaokoa wote wanaomjia Mungu kwa nia yake!TVV 425.1

    “Amini nakuambia leo hivi, utakuwa pamoja nami peponi.” Kristo hakumwahidi yule mwizi kuwa atakuwa pamoja naye peponi siku hiyo. Yeye mwenyewe hakuenda peponi siku hiyo. Alilala kaburini, na asubuhi ya siku ya kufufuka, alisema, “Sijapaa kwenda kwa Baba yangu bado.” Yohana 20:17. Lakini katika siku iliyoonekana ya kushindwa, ahadi ilitolewa. “Leo” wakati akifa msalabani kama mwizi, Kristo alimhakikishia mwenye dhambi, “Utakuwa pamoja nami peponi.” Mahali Kristo alipowekwa msalabani katikati ya wale wezi, palipangwa na makuhani na wakuu, kuonyesha kuwa alikuwa mhalifu mkuu kati yao watatu. Lakini jinsi alivyowekwa “katikati” vivyo hivyo msalaba wake ulisimikwa katikati ya ulimwengu unaokufa dhambini. Na maneno ya msamaha yaliyosemwa kwa yule mwizi aliyetubu, yaliwasha mwali wa nuru itakayong’aa mpaka kufikia pande zote za ulimwengu.TVV 425.2

    Katika kudhalalishwa kwake, Yesu kama nabii alikuwa amewazungumza na binti za Yerusalemu; kama kuhani na mwombezi alikuwa amemsihi Baba awasamehe wauaji wake; na kama Mwokozi alikuwa amesamehe dhambi za yule mwizi aliyetubu. Chini ya msalaba mama yake alisimama akiegemea kwa Yohana. Hakuweza kuvumilia kuwa mbali na mwanawe, na Yohana akijua ya kuwa mwisho uko karibu, alikuwa amemleta tena. Akiutazama uso wenye majonzi alimwambia; “Mama tazama mwanao.” Kisha akamwambia Yohana: “Tazama, mama yako.” Yohana alielewa na akaukubali wajibu huo. Tangu wakati huo Yohana alimchukua na kumtunza kwa huruma. Mwokozi hakuwa na fedha za kumhifadhia mama yake, lakini alitoa kile alichokihitaji sana huruma za mtu aliyempenda kwa sababu alimpenda Yesu. Na Yohana alipata mbaraka mkubwa kwa sababu Mariamu daima alinikumbusha Bwana wake mpendwa. Kwa muda wa miaka karibu thelathini Yesu alimhudumia katika kazi za nyumbani. Na sasa hata katika taabu yake ya mwisho alimfikiria mama yake mjane mwenye huzuni. Wale wanaomfuata Yesu watawaheshimu na kuwatunza wazazi wao. Kutoka katika moyo ambapo upendo wake unathaminiwa, baba na mama hawatakosa matunzo na huruma ya upendo. Na sasa Bwana wa utukufu alikuwa karibu kufa. Yote yalikuwa ni huzuni tupu. Siyo hofu ya kifo, wala ya maumivu ya msalaba iliyosababisha uchungu moyoni mwake. Mateso yake yalitokana na ubaya wa dhambi. Kristo aliona jinsi ambavyo ni watu wachache watakaoweza kuzishinda nguvu zake. Bila ya msaada kutoka kwa Mungu, wanadamu wataangamia tu, na aliona maelfu wakiangamia huku wakiwa karibu na msaada.TVV 426.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents