Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Yesu aliponya kwa makusudi siku ya Sabato

    Dhabihu zenyewe kama zilivyo hazikuwa na maana yoyote. Zilikuwa njia tu sio mwisho. Kusudi la dhabihu ilikuwa ni kuwaelekeza watu kwa Mwokozi, ili kuwaleta watu wapatane na Mungu. Ni huduma ipendezayo kwa Mungu hasa. Huduma hii inapokosa kuwa na umuhimu wake, huwa machukizo kwa Mungu. Ndivyo ilivyo na Sabato pia. Mawazo ya watu yanapojawa na wasiwasi na mizigo yenye kuleta mashaka kunabaki tu kuishika kisheria makusudi ya Sabato hupotoshwa. Kuishika tu kisheria ilikuwa kukufuru.TVV 155.1

    Siku nyingine ya Sabato, Yesu aliona katika sinagogi mtu mmoja mwenye mkono umepooza. Mafarisayo walitazama kwa makini waone jinsi Yesu atakavyofanya. Mwokozi hakusita kuondoa ukuta wa mapokeo yao ya kuifanya Sabaato kuwa mwiko usiofaa.TVV 155.2

    Yesu alimwamuru yule mwenye dhiki kusimama, halafu aliuliza swali: “je ni halali kutenda mema siku ya Sabato, au kutenda mabaya, kuokoa maisha au kuangamiza?” Marko 3:4. Ilikuwa kawaida kwa Wayahudi kwamba, mtu anaposhindwa kutenda mema anapokuwa na nafasi ya kutenda hivyo, ilikuwa vibaya, kutojali kuokoa katika hali yao hasa. “Lakini wao walinyamaza kimya katika swali lake. Naye aliwaangalia kwa ghadhabu, hali akisikitika kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akasema: “Nyosha mkono wako.” Akanyosha mkono wake, akawa mzima” Fungu 5. Yesu alipoulizwa kuwa: “Ni halali kuponya siku ya Sabato?” Alijibu: “Ni mtu gani wa kwenu akiwa na kondoo aliyetumbukia shimoni siku ya Sabato asiyemwinua na kumtoa humo? Mtu ana thamani kubwa kiasi gani kuliko kondoo! Basi ni halali kutenda mema siku ya Sabato.” Mathayo 12:10-12.TVV 155.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents