Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Namna tunavyorudia kutoamini kwa Adrea

  Kristo ametuagiza akisema: “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri injili kwa kila kiumbe.” Marko 16:15. Lakini ni mara ngapi sisi tunakata tamaa, tunapoona ukubwa wa kazi, na udogo wetu wa kuweza kuikamilisha. Sawa kama Andrea, hata sisi husitasita, na hatuwei tayari kutoa vyote tulivyo navyo ili kuwapa wengine chakula. Lakini yesu hutuagiza na kusema: “Wapeni ninyi chakula.” Nyuma ya agizo lako kuna uwezo wa kuwalisha makutano ya watu.TVV 204.5

  Katika tendo la Kristo kumefungwa fundisho kwa ajili ya waatendakazi wakee. Kristo alipokea kutoka kwa Baba, akawapa wanafunzi wake; nao wakawagawanyia makutano, na kwa watu, kila mtu. wote wanaounganika na Kristo watapokea kwake mkate wa uzima, na kuwagawanyia wengine. Yesu alitwaa mikate midogo, na ingawa ilikuwa sehemu ndogo aliyoawapa wanafunzi wake, hakutaka waile; ila waigawanye kwa makutano. Chakula kilichoongezeka mikononi mwake, na mikononi mwa wanafunzi wake kiliyotoka kwa Kristo, hakikuwa kidogo. Baada ya watu kula, Kristo na wanafunzi wake nao wakala pamoja chakula kilichoongezeka kwa nguvu za mbinguni.TVV 205.1

  Wanafunzi ndio walikuwa njia ya mawasiliano, kati ya watu na Kristo, jambo hili ni la kutia moyo sana kwa wanafunzi wa Yesu siku hizi. Sisi tunaweza kutoa kile tulichopokea kutoka kwa Kristo, na sisi tunaweza kupokea tu kadiri lunavyotoa kwa wengine. Kadiari tunavyotoa sana ndivyo tutakavyopokea zaidi.TVV 205.2

  Mara nyingi mtendakazi wa Kristo hushindwa kufahamu madaraka yake. Huwa na hatari kuelekeza na kutoa wajibu wake na kulitwika shirika, badala ya kumtegemea mwenye uwezo wote. Kazi yenye kufaulu, ambayo ni kazi ya Kristo, haitegemei talanta mtu aliyojifunza na njia za kufanyia kazi mtu alizojifunza, ila hutegemea imani. Badala ya kutupa wajibu unaokupasa kwa mtu mwingine unayedhani kuwa anao uwezo zaidi yako, fanya kazi kwa kadiri ya uwezo wako. Unapopata swali moyoni mwako kuwa, “Tunanunua wapi mikate ya kuwatosha watu waote hawa?” Jibu lako lisiwe la kutoamini, ila lenye imani. Wakati watu wanapokosa kuwa na mkate wa uzima, je tumtume mtu kutoka mbali aende kuwalisha? Kristo alisema: “Waketisheni watu, mkawalishe.” Vivyo hivyo, unapuzungukwa na watu wenye njaa, fahamu kuwa Kristo yuko hapo. Leta vipande vyako kwa Yesu. Vichache vinavyotumiwa katika kazi ya Yesu kwa hekima, vitaongezeka wakati wa kuwapa watu.TVV 205.3

  Bwana husema, “Toeni, nanyi mtapewa.” Yule anayezidisha mbege za manzi, na mikate kwa walaji, ndiye atazidisha uwezo wako, nawe utapata mavuno ya haki. Utatajirishwa kwa kila njia wakati unapokuwa mkarimu. Tazama Luka 9:10, 11.TVV 205.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents