Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wema wa Yesu kwa Pilato

  Pilato alishtushwa isiwe kwamba anayesimama mbele yake ni mtu kutoka mbinguni! Kwa mara nyingine tena akamwambia Yesu “Wewe umetokapi?” Lakini Yesu hakumjibu. Mwokozi alikuwa amezungumza na Pilato wazi, na kumweleza kazi yake. Pilato alikuwa amepuuza nuru. Alikuwa amedharau cheo cha uhakimu kwa kuitikia matakwa ya watu wenye makelele. Yesu hakuwa na nuru zaidi kwa Pilato. Akichukizwa na ukimywa wake, Pilato alisema kwa kiburi: “Husemi nami? Hujui ya kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua, nami nina mamalaka ya kukusulibisha?”TVV 416.6

  Yesu akamjibu, “Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu, kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi.” Kristo alimaanisha Kayafa, aliyekuwa akiliwakilisha taifa zima la Wayahudi. Walikuwa na nuru katika unabii uliomshuhudia Kristo, na ushahidi dhati kuhusu Uungu wake yeye waliyemhukumu kifo. Jukumu kubwa zaidi liliwaangukia wale waliokuwa viongozi wa taifa. Pilato, Herode na, askari wa Kirumi hawakumwelewa Yesu. Hawakupata nuru kama ile taifa la Kiyahudi liliyoipata. Kama askari wale wangalipata nuru hiyo wasingalimtendea Yesu jinsi hiyo.TVV 417.1

  Kwa mara nyingine tena Pilato akapendekeza kumwachia Mwokozi. “Lakini Wayahudi wakapiga makalele wakisema, Ukimfungua huyu, wewe si rafiki yake Kaisari.” Katika watu wote waliowapiga Warumi, Wayahudi walikuwa wakiwachukia kabisa; lakini kwa kutaka kukamilisha makusudi yao ya kumwua Yesu, walijifanya kuwa waaminifu kwa utawala huo wa kigeni, waliouchukia.TVV 417.2

  Waliendelea kusema, “kila mtu ajifanyaye kuwa mfalme, humfitini Kaisari.” Pilato alikuwa anatiliwa mashaka na Warumi na alijua kuwa habari kama hizo zikisikika ataangamia. Alijua kuwa Wayahudi hawataachia cho chote kile katika kutekeleza azima yao ya kulipiza kisasi.TVV 417.3

  Tena Pilato akamweka Yesu mbele ya watu akisema, “Tazama, Mfalme wenu!” Mara hii tena kelele za wazimu zilisikika zikisema: “Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe!” Kwa sauti iliyosikika mbali na karibu Pilato akauliza, “Je! nimsulibishe mfalme wenu!” Lakini kutoka katika midomo ya matusi, kufuru yalisikika yakisema: “Sisi hatuna mfalme, ila Kaisari.”TVV 417.4

  Hivyo kwa kuchagua mtawala wa kishenzi Wayahudi walimkataa Mungu asiwe Mfalme wao. Tangu hapo hawakuwa na mfalme, ila Kaisari. Hivyo ndivyo makuhani na walimu walivyowaongoza watu kufanya. Kwa sababu hiyo waliwajibika, na matokeo yakutisha yaliyofuata. Dhambi na aangamio la taifa vilisababishwa na viongozi wa dini.TVV 417.5

  “Basi Pilato alipoona ya kuwa haifai lo lote, bali ghasia inazidi tu, akatwaa maji, akanawa mikono mbele ya mkutano akasema, Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe.” Pilato akamtazama Mwokozi, na kusema moyoni mwake kuwa huyu ni Mungu. Akawageukia watu, akisema: Mimi sina hatia kwa damu yake. Msulibisheni, lakini natamka kuwa ni mwenye haki. Naye anayemtaja kuwa Baba yake awahukumu ninyi na siyo mimi kwa kazi hii ya leo. Halafu akamwambia Yesu, Nisamehe kwa kitendo hiki; siwezi kukuokoa. Na baada ya kumpiga Yesu mjeledi, akamtoa ili asulibiwa.TVV 418.1

  Pilato alitamani kumwokoa Yesu, lakini aliona kuwa hawezi kufanya hivyo na kubakia katika cheo chake. Kuliko kupoteza mamlaka yake ya ulimwengu, alichagua kumtoa kafara mtu asiye na kosa. Na watu wangapi hutupilia mambo ya ukweli kwa jinsi hii. Dhamiri na wajibu huelekeza njia moja, na kujipenda nafsi huelekea njia nyingine. Mkondo huelekezwa upande mpotovu, na yeye anayeridhia na uovu hukokotwa kupelekwa katika giza la hatia.TVV 418.2

  Lakini licha ya tahadhari yake, jambo lile aliloogopa Pilato lilimpata. Aliangushwa kutoka katika cheo chake, na akiumia kwa masikitiko na machozi haukupita mda mrefu baada ya kusulibishwa Kristo, alijiua mwenyewe.TVV 418.3

  Wakati Pilato aliposema kuwa hana hatia ya damu ya Kristo, Kayafa alijibu kwa kiburi: “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu.” Maneno yale yaliitikiwa na mkutano wote kwa mngurumo wa sauti zizizo za kibinadamu. Umati wote ukasema, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu.”TVV 418.4

  Wana wa Israeli walikuwa wamefanya uchaguzi waoBaraba ambaye alikuwa haramia, na mwuaji mjumbe wa Shetana. Kristo, mjumbe wa Mungu alikataliwa. Katika kufanya uchaguzi huo, walimkubali yule ambaye tangu mwanzo alikuwa mwongo na muuaji. Shetani akawa kiongozi wao, na utawala wake utawaendesha.TVV 418.5

  Wayahudi walikuwa wamepiga kelele: Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu”. Ombi lao lilijibiwa Damu ya Mwana wa Mungu ilikuwa juu ya watoto wao na juu ya wajukuu wao. Katika tukio la kutisha ombi lao hilo lilitimizwa wakati wa uharibifu wa Yerusalemu na hali ya taifa ya Kiyahudi kwa karibu miaka elfu mbili iliyofuata tawi lililokatwa kutoka katika mzabibu lilikauka. Kutangatanga kwao toka nchi hata nchi na toka kizazi hata kizazi wakifa katika uasi na dhambini!TVV 418.6

  Katika hali ya kutisha ombi hilo litatimzwa katika siku ile ya hukumu ya mwisho. Kristo atakuja katika utukufu wake. Maelfu na maelfu ya malaika, wana uzuri wa Mungu walishinda, wataamsindikiza naye njiani. Watu wa mataifa yote watakusanywa mbele yake. Badala ya taji ya miiba atavaa taji ya utukufu. Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na katika paja lake: “MFLME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.” Ufunuo 19:16.TVV 419.1

  Makuhani na wakuu wataliona tena matukio lile la jumba la hukumu. Kila jambo litaonekana kana kwamba limechorwa kwa herufi za moto. Kisha wale waliomba, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu,” watapokea jawabu la ombi lao. Kwa uchungu wa kutisha na wa kuogofya watalilia miamba na milima, Tuangukieni. (Tazama Ufunuo 6:16, 17).TVV 419.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents