Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  32 — Afisa wa Jeshi Aomba Msaada Kwa Ajili Mtumishi Wake

  Kristo alikuwa na masikitiko kwa vile taifa lake mwenyewe lilikuwa likitaka kuona ishara ndipo likiri kuwa alikuwa Masihi Lakini alishangaa kwa kuwona akida akija kwake, wala si0 kumwomba aende nyumbani kwake ili akafanye mwujiza wa kuponya, ila alisema “Sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.”TVV 170.1

  Mtumishi wa akida alikuwa na ugonjwa wa kupooza. naye alikuwa katika hali ya kufa. Baadhi ya watumishi wa Warumi walikuwa watumwa, ambao walikuwa wakinunuliwa na kuuzwa, na kutendewa ukatili mkubwa, hali wakidharauliwa. Lakini Akida huyu alikuwa akimtendea mtumishi wake kwa fadhili sana, kwa hiyo alikuwa akitamani apone. Aliamini kuwa Yesu aliweza kumponya Habari za Yesu alizosikia zilimpa tumaini Mrumi huyu alikubali kuwa dini ya Wayahudi ilikuwa bora zaidi kuhko dini yake. Alikuwa ameacha chuki iliyokuwapo kati ya Wayahudi na Warumi; naye aliwapenda Wayahudi. Katika mafundisho ya Kristo alipata kuu ambacho mtu huhitaji. Mambo vote ya kiroho aliyokuwa nayo yalikubaliana na maneno ya Mwokozi Lakini alijiona kuwa hastahili kufika mbele zake. Kwa hiyo aliwauhza wazee wa Kiyahudi wamwombee kuhusu mtumishi wake. Walikuwa wamezoeana na Mwalimu huyu Mkuu, kwa hiyo wangaliweza kujua iinsi ya kumfikia, na kumvutia. Yesu alipoingia Kapernaumu alikutana na kikundi cha wazee. Wakaeleza kuwa wanamjua, na wakasema kuwa yeye anastahili kutendewa fadhili; maana anaPenda taifa letu, naye ametujengea sinagogi.TVV 170.2

  Mara moja Yesu aliondoka kwenda kwa akida huyo. lakini kwa kusongwa na makutano ya watu, mwendo wake ulikuwa wa pole ppole. Akida akiwa na wasiwasi alimtumia ujumbe kwamba: “Bwana . . . sistahili wewe uingie nyumbani mwangu ” Lakini Mwokozi aliendelea na safari yake tu. Akida baadaye akimkaribia, alisema. Wala sistahili kuja mbele yako.” “Sema neno lako tu na mtumishi wangu atapona. Maana mimi pia ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, nina askan chini yangu, nikimwambia huyu “Nenda huenda. na huyu njoo, huja, na kwa mtumishi wangu, fanya hivi hufanya. Kama ninavyowakilisha serikali ya Kirumi, ndivyo hata wewe huwakiliksha uwezo wa Mwenyezi Mungu; na viumbe wote hutii amri zako. Unaweza kuag a ugonjwa ukaondoka, na utatii neno lako. Unaweza kuamuru watumishi wa mbinguni wakaleta nguvu za kuponya. “Sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.TVV 170.3

  Yesu aliposikia hivyo, alistaajabu, akawageukia watu waliomfuata, akawaambia: “Amin nawaambieni, sijaona imani kubwa, katika Israeli.” na kwa akida alisema, “Kama ulivyoamini, iwe hivyo kwako. Mtumishi wake akapona saa ile ile.”TVV 171.1

  Katika upofu wao wa kuwa na haki yao wenyewe. Waahudi walimsifu akida kwa ajili ya wema aliowafanyia kama taifa. Lakini akida alijisema mwenyewe kuwa “hastahili.” Hakutumainia wema wake. Alimwamini Kristo tu ambaye ni rafiki na Mwokozi wa wanadamu.TVV 171.2

  Wakati Shetani anakuambia ya kuwa u mwenye dhambi, mwambie kuwa Kristo alikuja ulimwenguni kuokoa wenye dhambi. Maombi tunayomwomba sasa huonyesha hali yetu ya kutoweza chochote, ambayo hufanya atusaidie kutoweza kwetu.TVV 171.3

  Mkononi mwangu hakuna bei ninayoletaTVV 171.4

  Msalabani mwako nashikiliaTVV 171.5

  Wayahudi hawakuona kitu chochote cha kumtamani Yesu Lakini akida, ambaye alifundishwa kat a shule za kimizimu za Rumi, ambaye alionekana kutengwa na hali ya dini ya Kiyahudi mtu huyu alipata ni kamili, ambayo watoto wa Ibrahim hawakuijua. Nuru iwamulikiayo watu wanaokuja ulimwenguni (Soma Yohana 1:9) imeng’aria mtu huyu, naye ameuona utukutu wa Mwana wa Mungu. Kwa Yesu mtu huyu alikuwa mavuno maalum ya watu kutoka katika mataifa, kuja katika ufalme wake.TVV 171.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents