Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mzigo wa dhambi

  Yesu hakufurahia kuponya watu miili tu, bali alifurahia kumwondoa mtu katika wasiwasi wa kulemewa na dhambi. Kama mtu angepata hakikisho la kusamehewa dhambi, angeridhika hata ikiwa ni kufa angekufa kwa tumaini. Mtu anayekufa hana wakati wa kupoteza. Aliwasihi rafiki zake wampeleke kwa Yesu hata kama ni kumbeba juu ya kitanda. Lakini pale Mwokozi alipokuwa palikuwa na watu wengi sana, hata haikuwezekana kwa mgonjwa na rafiki zake kufika karibu, au kiasi cha kusikia sauti yake.TVV 144.4

  Yesu alikuwa akifundisha nyumbani kwa Petro, Wanafunzi wake walikuwa karibu naye. Palikuwa na Mafarisayo na wataalam wakiketi karibu naye, nao walitoka katika miji yote ya Galilaya, na Uyahudi na Yerusalemu, kama wapelelezi. Huko nje walikusanyika watu wengi, wenye kutaka kusikia, wanyenyekevu, wachunguzi wa mambo, na wasiamini. Uwezo wa Bwana wa kuponya ulikuwa unafanya kazi. Lakini Mafarisayo na Walimu wakuu hawakukutambua kuwako kwa Roho wa Bwana. Hakuwa na haja yoyote maana hawakuhusika na uponyaji huo. Aliwashibisha wenye njaa ya haki na mambo mazuri, ila matajiri, ambao hawakuwa na haja yoyote, walikwenda zao watupu. Luka 1:53.TVV 144.5

  Waliomchukua mwenye kupooza walijaribu kuwasukuma watu ili wapate nafasi ya kupita, lakini hawakufaulu. Mgonjwa atakata tamaa? Akawashauri waliomchukua wampitishe juu ya paa la nyumba, wavunje mahali na kumtelemsha chini katika miguu ya Yesu.TVV 145.1

  Mwokozi aliona macho yenye machozi akaelewa maana yake. Wakati mgonjwa huyu alipokuwa angali nyumbani, alikirishwa moyoni juu ya uwezo wa Yesu wa kuponya. Alipoungama dhambi zake, rehema za kuponya za Mwokozi zilimtia changamko rohoni.TVV 145.2

  Sasa maneno ya Mwokozi yalisema kwake: “Mwana . . . dhambi zako zimesamehewa.” Hali yake ya kukata tamaa ikatoweka, hali ya kusamehewa na tumaini lake ikang’aa moyoni mwake. Maumivu yake yakatoweka, hali yake ya afya ikamrudia. Mgonjwa wa kupooza akaponywa, mzigo wa dhambi zake ukasamehewa.TVV 145.3

  Kwa maneno machache ya imani aliyaamini maneno ya Yesu. Wala hakutaka kuomba kitu zaidi. Akajazwa na furaha kuu aliondoka watu wakimwangalia kwa hofu.TVV 145.4

  Marabi walikumbuka jinsi mtu huyu alivyowafikia akitaka msaada, nao hawakuweza kumpa msaada wowote, akasema kuwa alikuwa akiugua ugonjwa wa laana ya dhambi. Wakaona mambo muhimu yanayotendwa na Yesu, na ya kwamba mvuto wake unazidi kuwa mkubwa kwa watu. Wakatazamana kwa mshangao. Wakaona kuwa ni lazima kufanya jambo fulani ili kuzuia mambo haya. Yesu ametangaza wazi kuwa mwenye kupooza amesamehewa dhambi zake Mafarisayo waliweza kusema kuwa, jambo hilo ni kufuru, ni kosa linalostahili kufa. Wakasema “Ni kufuru! Ni nani awezaye kusamehe dhambi, isipokuwa ni Mungu mwenyewe.”TVV 145.5

  Yesu akiwakazia macho, alisema: “Kwa nini mnawazawaza mioyoni mwenu? Ni jambo gani jepesi kumwambia mwenye kupooza, Dhambi zako zimesamehewa, au kusema, Ondoka ujitwike kitanda uende zako? Lakini mjue kuwa Mwana wa Adamu anao uwezo wa kusamehe dhambi. Akamwambia mwenye kupooza, Nakuambia ondoka, ujitwike kitanda chako uende zako nyumbani.”TVV 145.6

  Ndipo mtu aliyekuwa amechukuliwa kwa machela, akasimama kwa miguu yake, akiwa na nguvu kamili kama kijana.TVV 145.7

  Kila kiungu mwilini mwake kikawa imara. Hali ya afya kamili ikawa badala ya hali ya unyonge na kifo. Mara moja akaondoka, akachukua kitanda akaenda zake mbele ya watu wote. Basi wote wakashangaa, wakamtukuza Mungu wakisema, Hatujaona jambo kama hili katika kizazi hiki.TVV 146.1

  Uwezo wa kuumba ulitia nguvu katika mwili uliooza. Uwezo ule ule uliosema kwa mtu wa kwanza aliyeumbwa kwa mavumbi ya nchi, ndio huo huo uliosema kwa mwenye kupooza . Uwezo uliotia uzima mwilini mwake, ndio uliotakasa moyo wake. Kristo alimwamuru mwenye kupooza, aondoke na kwenda ili watu wajue kuwa Mwana wa Adamu anao uwezo wa kusamehe dhambi duniani.TVV 146.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents