Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mungu Peke Yake Aweza Kusamehe

    Ni kwa njia hii tu ndiyo kanisa linakuwa na uwezo wa kumwondolea dhambi mwenye dhambi. Ondoleo la dhambi linaweza tu kupatikana kwa sifa njema za Kristo. Uwezo wa kusamehe dhambi haukutolewa kwa mtu yeyote, au kwa kundi fulani la watu. Jina la Yesu ndilo jina pekee “chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” Mdo 4:12.TVV 455.2

    Mara ya kwanza Yesu alipokutana na wanafunzi katika chumba cha ghorofa, Tomaso hakuwako. Alisikia kutoka kwa wengine kwamba Yesu amefufuka, lakini huzuni na kutoamini vilijaza moyo wake. Ikiwa Yesu amefufuka kweli, hakutakuwa na tumaini la ufalme wa duniani. Na ilimuudhi kufikiria kwamba Bwana wake afufuke na kujidhihirisha kwa wengine wote isipokuwa yeye. Kwa hiyo aliamua kutoamini, na kwa juma zima alinung’unikia huzuni yake.TVV 455.3

    Alirudia mara kwa mara akisema: “Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo.” Hakutumia imani kutokana na ushuhuda wa ndugu zake. Alimpenda Bwana wake lakini aliruhusu wivu na mashaka yajae moyoni mwake.TVV 455.4

    Siku moja jioni Tomaso alikusudia kukutana na wenzake katika chumba cha ghorofa. Alikuwa na tumaini kidogo sana kwamba kuwa habari hizo zilikuwa za kweli. Wakiwa wanakula chakula cha jioni, walikuwa wanaongea kuhusu ushahidi wa unabii alioutoa Kristo. “Kisha Alikuja Yesu na milango imefungwa, Akasimama katikati Akasema; Amani iwe kwenu.”TVV 455.5

    Akamgeukia Tomaso na kusema; “Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu lete na mkono wako uutie ubavuni mwangu; wala usiwe asiyeamini bali aaminiye”. Mwanafunzi mwenye mashaka alijua kuwa hakuna mwanafunzi mwingine ambaye angeweza kumwambia Bwana juu ya kutoamini kwake. Hakuwa na haja tena ya ushahidi zaidi. Moyo wake ukafurika kwa furaha, na akaanguka miguuni pa Yesu akilia: “Bwana wangu na Mungu wangu!”TVV 456.1

    Yesu alipokea ungamo lake, lakini kwa upole akakemea kutokuamini kwake: “Tomaso, wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.” Ikiwa ulimwengu sasa utafuata mfano wa Tomaso, hakuna mtu atakayeamini, kwa maana wote wale wanaompokea Kristo lazima wafanye hivyo kwa ushuhuda wa wengine. Wengi ambao, kama Tomaso hungojea mpaka kila shaka limeondolewa kamwe hawatafikia tumaini lao. Kwa taratibu huthibitika katika kutoamini kwao. Wanapanda mbegu za mashaka, na watavuna mashaka yao. Wakati imani na matumaini ni ya muhimu, wengi watajikuta pasipo kuwa na nguvu za kutumaini na kuamini.TVV 456.2

    Jinsi Yesu alivyomtendea Tomaso huonyesha namna ambavyo tunapaswa kuwatendea wale wanaokuza mashaka yao. Tomaso hakuwa na busara katika kuweka masharti ya imani yake, lakini Yesu, kwa wema wake alivunjilia mbali vizuizi vyote. Kwa nadra sana kutoamini huondolewa kwa mabishano. Lakini hebu mruhusu Yesu, katika upendo wake na rehema, adhihirishwe kama Mwokozi Aliyesulibishwa, na kutoka katika midomo ambayo hapo kwanza haikuwa tayari kusikike ungamo la Tomaso, “Bwana wangu na Mungu wangu.”TVV 456.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents