Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Je, Yesu alidai yasiyowezekana?

  Kijana tajiri mtawala alifahamu maana ya maneno ya Yesu, kwa sababu alikwenda zake kwa huzuni. Alikuwa mmojawapo wa wabunge wa Kiyahudi, na Shetani alikuwa akimjaribu apate kujivunia hali yake ya baadaye. Alitaka hazina ya mbinguni, lakini pia alitaka kile ambacho utajiri wake utakachomfanyia duniani. Alitamani uzima wa milele lakini pia aliona kuwa kuuza vitu vyake ni kujitolea kukubwa kabisa, kwa hiyo alikwenda zake kwa huzuni, kwa “kuwa alikuwa na mali nyingi.”TVV 293.5

  Kule kujigamba kwamba ameshika amri za Mungu tokea utoto wake, kulikuwa kwa uongo. Ilionyesha kwamba utajiri ndio uliokuwa sanamu yake. Alipenda kipawa cha Mungu zaidi kuliko kumpenda mwenye kumpa kipawa. Kristo alimwambia kijana huyu amfuate. Alisema: “Nifuate.” Lakini Mwokozi hakuwa na thamani kwake, kuliko jina lake na mali zake vilivyokuwa na thamani mbele ya watu. Kukubali vitu visivyoonekana na kuacha vitu vinavyoonekana, kwake lilikuwa jambo zito. Alikataa uzima wa milele, akaenda zake. Hata ulimwengu kamwe haumkubali. Watu maelfu huchagua ulimwengu na mambo yake kuliko Kristo.TVV 294.1

  Jinsi Kristo alivyoshughulika na kijana huyo ni fundisho kubwa. Mungu ametupa kanuni, ambazo wafuasi wake lazima wazifuate. Ni kuzitii amri zake, sio kuzikariri tu. Ni utii unaoonekana katika maisha ya kubadili tabia. Bwana husema: Watakaosema kuwa vitu vyangu vyote na mimi ni wake, ndio watakaotambuliwa kama wana wa Mungu. Mwokozi hutaka tushirikiane naye kufanya kazi ya Mungu, kwa njia hii tu tutaokolewa.TVV 294.2

  Mungu amewapa watu mali, talanta, na nafasi ili wawe wajumbe wake wa kuwasaidia maskini na wahitaji. Anayetumia mali yake kama Mungu alivyotaka huwa mkazi pamoja naye.TVV 294.3

  Wale wenye mali na wakuu duniani, kama yule kijana huona kuwa Mungu huwadai mno kupita kiasi, kwa hiyo huenda zao kwa huzuni. Hakuna utii wa nusu nusu utakaokubaliwa mbele za Mungu. Hakuna njia ya kumwokoa mtu, ila kuacha yote yanayoleta laana.TVV 294.4

  Wafuasi wa Kristo wanapomtolea Bwana mali yake, huweka hazina mbinguni, ambayo watapewa watakaposikia sauti: “Vema .... Ingia katika furaha ya Bwana wako.” Mathayo 25:23. “Furaha ya kuwaona waliokombolewa kwa wote waliojitia kazini mwa Bwana, aliyesema: ‘Nifuate.”TVV 294.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents