Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mzigo wa Kuogofya Alioubeba Kristo

  Juu ya Kristo ambaye ni badala yetu na mdhamini wetu yalitwikwa maovu yetu yote. Hatia ya kila mzao wa Adamu, iliuelemeza moyo wake. Katika maisha yake yote, Kristo alikuwa akitangaza habari njema ya msamaha wa upendo wa Baba, lakini sasa akiwa amelemewa na uzito wa hatia ya ulimwengu hakuweza kuuona uso wa upatanisho wa Baba. Hili liliuchoma moyo wake kwa uchungu usioweza kueleweka kwa mwanadamu. Uchungu huu wa rohoni ulikuwa mkubwa mno kiasi kwamba maumivu ya mwilini hayakuweza kusikika.TVV 426.2

  Shetani alisonga moyo wa Yesu kwa majaribu makali Tumaini halikuonyesha kufufuka kutoka kahurim kama mshindi au kumjulisha kuwa amekubalika na Baba.TVV 427.1

  Kristo alisikia uchungu ule wenye dhambi watakaosikia wakati ule huruma zitakapokoma kuwatetea wenye dhambi. Ilikuwa ni ile hali ya dhambi, iliyoleta ghadhabu ya Baba dhidi yake akiwa badala ya mwanadamu, ndiyo iliyoupasua moyo wa Mwana wa Mungu.TVV 427.2

  Majeshi ya mbinguni yalifunika nyuso zao wasione lile tukio la kutisha. Jua pia lilikataa kuangalia hali hiyo ya kutisha. Nuru yake ilikuwa ikimulika dunia wakati wa adhuhuri wakati ilipozimika ghafla. Kukawa giza kamili lilifunika msalaba. “Palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa.” Hapakuwa na sababu za kawaida kuhusu giza hilo ambalo lililokuwa nene kama giza la usiku wa manane usiokuwa na mbalamwezi au nyota. Ulikuwa muujiza uliotolewa na Mungu ili kwamba imani ya vizazi vijavyo ithibitike.TVV 427.3

  Katika giza hilo nene kuwako kwa Mungu kulifichika. Mungu na malaika watakatifu walikuwako kando ya msalaba. Baba alikuwa pamoja na Mwanawe. Lakini kuwako kwake hakukufunuliwa. Katika saa hiyo ya kutisha Kristo hakupaswa kufarijiwa kwa kuwako kwake Baba. Katika giza hilo nene kuwako kwa Mungu kulifichika. Mungu pamoja na malaika watakatifu walikuwepo kando ya msalaba. Wote waliomwona Kristo katika mateso yake walisadikishwa juu ya Uungu wake. Wakati wote wa maumivu yake, alikuwa akitazamwa na umati uliomzomea. Sasa kwa rehema za Mungu alifichwa kwa vazi la Mungu.TVV 427.4

  Hofu isiyosemeka iliwapata wale waliokuwa pale msalabani. Mizaha na matusi vilikoma. Radi ilimulika mara kwa mara kutoka katika wingu na kumfanya Mkombozi aliyesulubiwa kuonekana. Makuhani, wakuu wanyongaji na ile halaiki wote wakidhani kuwa siku ya upatilizo wao imefika. Wengine walinong’ona kuwa sasa Yesu atatelemka kutoka msalabani. Panapo saa tisa giza likatoweka sehemu waliyokuwa watu, ila likawa bado linamzunguka Mwokozi. Hakuna jicho lililoweza kupenya utusitusi ulioifunika roho iliyoteseka ya Kristo. Kisha “Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akasema, Eloi, Eloi, lama sabakthani?” yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Wengine wakasema kuwa adhabu ya mbinguni inamkalia kwa sababu alijiita kuwa Mwana wa Mungu! Wengi waliomwamii walisikia kilio chake cha kukata tamaa. Matumaini yakawatoka. Ikiwa Mungu amemwacha Yesu, wafuasi wake watatumaini nini?TVV 427.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents