Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ufalme wenye Kanuni Tofauti

  Kristo alikuwa, akisimamisha ufalme wenye kanuni tofauti. Aliita watu, si wawe wakuu wa madaraka, ila wawe wahudumu, watu wenye nguvu za kuwategemeza wanyonge. Madaraka, vyeo, elimu, huwekwa chini ya huduma.TVV 306.6

  “Mwana wa Adamu hakuja kuhudumiwa, bali kuhudumu, na kutoa, maisha yake kuwa fidia ya wengi.” Kanuni ambayo Kristo aliyoweka ni ya kuliongoza kanisa ambalo ni mwili wake katika ufalme wa Kristo, wale wenye kufuata kielelezo chake ndiyo wakuu, wenye cheo.TVV 306.7

  Maneno ya Paulo yanadhihirisha ukuu wa hakika ambao ndio ukristo halisi. Paulo asema: “Ijapokuwa mimi ni huru kwa watu wote, lakini nimekuwa mtumwa wa wote. Sitafuti faida yangu mwenyewe, ila faida ya wengi, ili wapate kuokolewa.’ 1 Wakorintho 9:19; 10:33.TVV 307.1

  Kwa habari ya dhamiri hakuna mtu anayeweza kumtawala mwingine na kumpangia mambo yampasayo kutenda. Mungu amempa kila mtu uhuru wa kufikiri na kuamua. Kadiri ya uamuzi wake. Katika habari za kanuni, Paulo asema: “Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.” Warumi 14:5. Malaika wa mbinguni hawaji hapa duniani kutawala, au kudai heshima, ila huja kushirikiana na kuwainua wanadamu.TVV 307.2

  Kanuni na mafundisho ya Kristo yalikaa katika mawazo ya wanafunzi wake wapendwa mpaka siku zake za mwisho. Uzito wa mahubiri ya Yohana ulikuwa: “Mapana, hii ndiyo habari mliyosikia tangu mwanzo, kwamba tupendane sisi kwa sisi.” “Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa Yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.’ 1 Yohana 3:11, 16.TVV 307.3

  Roho ya namna hii ndiyo ilikuwako katika kanisa la kwanza baada ya kumwagwa kwa Roho Mtakatifu “Watu walioamini walikuwa na mojamoja na roho moja.” Mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi kwa.” Matendo 4:32, 33.TVV 307.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents