Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jiwe geni lilokuwa mfano wa Kristo

    Mwokozi akiwaangalia kwa masikitiko, alisema: “Hamkusoma kwamba jiwe lililokataliwa na waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni? Hii ni kazi ya Bwana, nayo imekuwa ajabu machoni mwetu?” Kwa hiyo nawaambieni, ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, litapewa taifa jingine lenye kuzaa matunda yake. Na ye yote aangukaye juu ya jiwe hili atavunjika vipande vipande; lakini yeye yule jiwe hili litakayemwangukia, litamsagasaga kuwa unga.”TVV 334.1

    Unabii huu ulikaririwa na Wayahudi mara kwa mara masinagogini mwao, ukimhusu Masihi ajaye. Kristo alikuwa Jiwe kuu la pembeni katika itikadi ya Wayabudi, na katika mpango mzima wa wokovu. Jiwe hili la msingi sasa lilikuwa linakataliwa na wajenzi wa Kiyahudi. Kwa kila njia na kwa bidii yote, Mwokozi alijitahidi kuonyesha maana ya matendo waliyokuwa wanataka kutenda. Kama wakishindwa kutubu kutokana na maonyo hayo yote, basi hukumu itawakumba, ajali ya Mungu katika kuwanyang’anya nafasi ya taifa lao na kisa cha kuwaacha na siyo tu kuliacha hekalu lao liharibiwe lakini kwa taifa lao kutawanywa.TVV 334.2

    Wasikiaji wake walifahamu maonyo hayo, lakini ya hukumu waliyojikatia wenyewe, licha makuhani na wakuu walikuwa tayari kujaza kikombe chao kwa kusema: “Huyu ndiye mrithi wa yote, haya na tumwue; “Lakini walipotaka kumkamata, waliogopa makutano, maana walikuwa upande wa Kristo.”TVV 334.3

    Kristo alipotaja juu ya unabii wa jiwe la msingi, lililokataliwa, alikuwa akisemea hekalu la kwanza. Jambo hili lilikuwa na maana kuhusu kuzaliwa kwake Yesu, lakini pia lina umuhimu na kwetu pia. Wakati hekalu la Sulemani lilipojengwa, mawe makubwa yaliandaliwa katika machimbo yake. Yalipoletwa mafundi waliyatia tu katika mahali pake. Kuhusu msingi, jiwe moja lilikuwa limeletwa na wajenzi hawakupata mahali pa kulitia. Jiwe hilo lililokosa mahali pake lilisumbua kuachwa tu pembeni. Hilo likabaki kama jiwe lililokataliwa.TVV 334.4

    Lakini wajenzi walipotafuta jiwe lifaalo katika hekalu la pili, iliwalazimu watafute na kuchagua jiwe lenye kufaa. Kama watatia jiwe lisofaa wangalileta uharibifu katika jengo. Lakini mwishowe walilirudia jiwe la kwanza walilolikataa. Lilipigwa na jua na baridi bila kupata nyufa. Baada ya kulijaribu lilionekana kuwa ndilo lifaalo. Jiwe hilo ni mfano wa Kristo.TVV 334.5

    Isaya asema: “Naye atakuwa ni mahali patakatifu bali ni jiwe la kujikwaza, na Mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili .... Na wengi watajikwaa juu yake, na kuanguka na kuvunjika, na kunaswa na kukamatwa.” Kristo atachukua majaribu yote ambayo jiwe la pembeni katika hekalu la Sulemani alikuwa mfano wake. “Tazama naweka jiwe katika Sayuni liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara, yeye aaminiye hatafanya haraka.” Isaya 8:14, 15; 28:16.TVV 334.6

    Mungu alichagua jiwe kuu la pembeni akaliita, “Msingi ulio imara.” Ulimwengu mzima unaweza kuweka juu yake uzito wake wote na matatizo yake yote. Vyote vya ulimwengu vitakaa juu yake bila kuuharibu. Wale wanaomtegemea hatawakatishwa tamaa. Yeye amejaribiwa katika mambo yote, akashinda. Amebeba kila mzigo uliowekwa juu yake na kila mtu atubuye. Wote wanaomtegemea yeye, hukaa salama kabisa. Kristo ndiye “Basi heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni. Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha. Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo” 1 Petro 2:7, 8.TVV 335.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents