Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Zakaria aliona shaka

  Zakaria aliona shaka kwa neno la malaika. Kwa hiyo alipigwa kuwa bubu mpaka kuzaliwa kwa mtoto. Malaika alisema: “Angalia utakuwa bubu mpaka kuzaliwa kwa mtoto, kwa sababu hukuyasadiki maneno yangu, ambayo yatatimia kwa wakati wake.” Katika huduma hii, ilikuwa kazi ya kuhani kuomba kwa ajili ya kusamehewa, na kwa ajili ya kuja kwa Masihi, lakini Zakaria alipojaribu kufanya hivyo, hakuweza kutamka neno. Alipotoka mahali patakatifu uso wake ulikuwa unang’aa kwa utukufu wa Mungu, na watu walidhani kuwa ameona njozi humo hekaluni. Zakaria alibaki kuwa bubu, ila alizungumza na watu kwa njia ya ishara tu, kuwaeleza mambo aliyoona na kusikia humo hekaluni.TVV 47.2

  Baada ya kuzaliwa mtoto aliyeahidiwa, ulimi wake ulifunguliwa. Mambo haya yote yalienea katika nchi yote ya Yuda, na wote walioyasikia waliyaweka katika mioyo yao, huku wakisema, “Mtoto huyu atakuwaje?” Mambo haya yote yahelekeza juu ya kuja kwa Masihi.TVV 47.3

  Roho Mtakatifu alimjaza Zakaria, naye akatabiri kuhusu kazi ya mwanae itakavyokuwa: “Wewe mtoto utaitwa nabii wake Aliye Juu, Maana utatangulia m bele ya Bwana ili kutayarisha njia yake. . . . Kutoa maarifa ya ukombozi kwa watu wake kwa njia ya kuondolewa dhambi zao.”TVV 47.4

  Mtoto akakua, akawa na nguvu rohoni, naye akawa jangwani mpaka siku ya kutokea kwake kwa Israeli.” Mungu alimkabidhi mwana wa Zakaria, kazi kubwa nmo, ambayo haijakabidhiwa kwa mtu yeyote. Na Roho wa Mungu atakuwa pamoja naye ikiwa atafuata maelekezo ya malaika.TVV 47.5

  Yohana alipaswa kuwaletea watu mwanga wa Mungu. Lazima awahakikishie haja yao ya kutaka haki ya Mungu. Mjumbe wa jinsi hiyo lazima awe mtakatifu, awe hekalu la Roho ya Mungu. Lazima awe na afya kamili, yaani afya ya mwili, ya roho, na ya mawazo. Kwa hiyo itampasa kutawala uchu wa chakula na tamaa.TVV 47.6

  Siku za Yohana mbatizaji, choyo cha kutajirika, na hali ya kupenda raha, na kujionyesha, ilikuwa imeenea sana. Tamaa ya mwili, ulevi, na kujifurahisha kwa sikukuu, vilidhoofisha mwili, na kudumaza mawazo, na kuelekeza mwili katika ufisadi. Katika hali ya kawaida, na mavazi ya kawaida tu, angekemea anasa na ufisadi wakati wake. Hayo ndiyo maelekezo malaika aliyoleta kutoka mbinguni.TVV 48.1

  Katika utoto wake na ujana wake, lazima ajizoeze kujitawala, na kuwa na uwezo kamili. Mazoea yanayopatikana tangu utotoni, ndiyo yatakayokuwa wakati wa utu uzima, kama atashinda, au atalegealegea. Ujana ni wakati wa kupanda mbegu, baadaye itaonekana aina ya mavuno yatakayotokea, katika maisha ya sasa na yale yajayo.TVV 48.2

  Katika kutayarisha njia kwa ajili ya kuja kwa Kristo mara ya kwanza, Yohana alikuwa mjumbe na kielelezo cha watu wanaotayarisha watu kwa ajili ya kurudi kwake Kristo mara ya pili.TVV 48.3

  Ulimwengu umezama katika anasa. Makosa na hadithi ni tele. Wote wanaojiandaa katika kumcha Mungu lazima wajifunze kuwa na kiasi, na kujitawala. Soma 2 Wakorintho 7:1. Uchu wa chakula pamoja na tamaa, lazima vitekwe nyara, na kutawaliwa na uwezo mkuu. Mawazo yatiishwe. Kujitawala kuwa ni kwa lazima, ndiko kutatuwezesha kuelewa na kutenda mambo ambayo ni sawa na kweli ya Mungu; kama neno lake lilivyo.TVV 48.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents