Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ushirikina ulikuza hofu

  Maonekano ya ushirikina na matendo yake huleta hofu kwa watu. Madhara zaidi hutokea kwa watu hawa wakiwa miongoni mwao. Waliovuka ziwa pamoja na Yesu walisimulia jinsi dhoruba ilivyokuwa, na jinsi mawimbi yalivyotulizwa. Lakini maneno yao hayakuwa na hatari. Ila kwa kushikwa na hofu ya washirikina, walimwomba Yesu aende zake; naye aliingia mashuani akaondo mara moja, akaenda ng’ambo.TVV 186.5

  Watu wa Gergasa waliogopa sana wasipoteze mali yao ya kidunia, kwamba yule alilyemwangamiza mkuu wa giza, alionekana machoni pao kama ni jasusi. Kipawa cha mbinguni kilipigwa marufuku kwao. Kulikuwa na wengi ambao hawakulipokea neno la Yesu kwa kuogopa kufilisika katika mali zao. Maana kulitii, kungehitaji kuacha mali zao. Walikataa kumkaribisha kwa kuogopa kuwa kutahitajika gharama zaidi za kuwakaribisha. Walikataa neema yake, wakamfukuza, atoke kwao.TVV 186.6

  Lakini wenye kuponywa mashetani walitaka kufuatana na Yesu, Mponya wao. Waliona kuwa kukaa na Yesu kutawaepusha na mashetani yaliyowasumbua. Yesu alipotaka kuingia mashuani wao waliandamana naye. Lakini Yesu aliwaambia waende nyumbani kwao, wakawaeleze watu wa kwao mambo makuu Bwana aliyowatendea.TVV 187.1

  Hapa walipewa kazi ya kufanya. Kwenda katika miji yao ya kimataifa wakawaeleze mibaraka waliyopata kutoka kwa Bwana. Ilikuwa vigumu sana kutengana na Yesu, ambaye ni Mponya wao. Kwa kuwa wametengana na watu wa kwao kwa siku nyingi sana, ilionekana kwao kuwa vigumu kutimiza kazi Yesu aliyowapa. Lakini mara ile Yesu alipotaja kazi yao, walikuwa tayaari kutii. Walikwenda katika Dekapoli yote, wakieleza mambo makuu Yesu aliyowafanyia, kwa kuwafungua kwa nguvu za mashetani. Katika k;klufanya kazi hiyo walipokea mibaraka mingi kuliko vile wangalikaa pamoja na Yesu. Kufanya kazi ya kueneza habari njema ya wokovu, hutuleta karibu na Mwokozi zaidi na zaidi.TVV 187.2

  Watu wawili walioondolewa mashetani walikuwa ndio wamisionari wa kwanza waliotumwa na Yesu kwenda kuhubiri injili huko Dekapoli. Watu hawa walimsikia Yesu akifundisha kwa muda mfupi sana. Lakini walikuwa na ushuhuda wa kuwaambia watu kuwa Yesu ndiye Masihi. Walisema kile walichojua, na kile walichoona, na kusikia; kuhusu uwezo wa Kristo. Haya ndiyo kila mtu anaweza kuyafanya kama ameguswa na upendo wa Mungu. Tazama 1 Yohana 1:1-3.TVV 187.3

  Tunapomfuata yesu hatua kwa hatua, tutakuwa na jambo la kusimulia katika maongozi yake maishani mwetu. Jinsi tulivyojaribu ahadi zake na kuziona ni za kweli. Huu ndio ushuhuda Bwana anatutaka tuutoe.TVV 187.4

  Ijapokuwa watu wa Gergesa hawakumpokea Yesu, hakuwaacha gizani. Hawakusikia maneno yake. Hawakujua lolote juu yake, kwa hiyo aliwatumia nuru kwa njia ya wale waliomkubali.TVV 187.5

  Kuangamia kwa nguruwe kuliwaamsha watu wote kuliko kitu kinginecho, kumwelekea Kristo. Watu walioponywa walikubali kuwa mashahidi wa uwezo wake, wakiwa mfereji wa nuru yake, na wajumbe wa Mwana wa Mungu. Milango ilifunguka katika nchi nzima. Yesu aliporudi Dekapoli watu maelfu walisikia neno lake. Hata watenda maovu pia hutumika kutenda mema.TVV 187.6

  Wenda wazimu wa Gergesa, waliokuwa wakiishi mapangoni, katika kifungo; katika tamaa zisizozuilika, huonyesha mambo ambayo Shetani huwatendea watu wanaojitolea katika njia zake. Mivuto ya Shetani kila mara huelekea kutawala nia na mawazo ya watu ili watende mambo yasiyosemeka. Hutia giza katika fahamu na kuvuruga nia ya mtu. Watu wanapokataa mwaliko wa Mwokozi, huwa wamejitolea katika mambo ya Shetani Watu maelfu katika miji yao, kazini, kwenye biashara, na popote pale, hufanya mambo kama haya siku hizi. Kwa ajili ya mambo haya, leo uasi umezidi duniani, na ufedhuli wa kila namna unawakumba watu. Shetani huwapeleka watu katika ubaya zaidi na zaidi, mpaka wameharibika kabisa kabisa. Usalama wa pekee ni kukaa pamoja na Yesu. Shetani amejionyesha mbele za malaika kuwa ni adui wa wanadamu, na mharibu wao. Na Yesu ni rafiki na Mwokozi wao.TVV 188.1

  Mungu ametuita tuwe, washiriki wa sura ya Mwana wake. Waarumi 8:29. Hata mtu aliyeazama na kuharibiwa na Shetani, katika Kristo, anaweza kuwa mtumishi wa haki, na aweza kutumiwa kwenda “Kutangaza mambo makuu ambayo Bwana amekufanyia.”TVV 188.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents