Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    16 — Kristo Akabili Machafuko Hekaluni

    Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu, na Yesu alipanda kwenda Yerusalemu. Yesu alikuwa bado kutangaza kazi yake waziwazi; kwa hiyo alijichanganya na kundi la watu bila kutambulikana. Nyakati kama hizi neno kuu la mazungumzo lilihusu kuja kwa Masihi. Yesu alijua kuwa tumaini la fahari ya taifa la Israeli litakatishwa tamaa, maana tumaini hili lilikuwa limejengwa kwenye tafsiri potofu ya Maandiko. Kwa juhudi kubwa alieleza jinsi unabii usemavyo, na akajaribu kuwafikirisha zaidi juu ya kuchunguza Neno la Mungu.TVV 80.1

    Wakati wa pasaka, watu wengi sana walikusanyika kutoka pande zote za Palestina, na nchi za kando yake. Sebule ya hekalu ikajaa tale kwa wingi wa watu. Wengi hawakuweza kuleta sadaka zilizotakiwa kutolewa kuwakilisha yule, ambaye ni sadaka halisi. Kwa ajili ya nafuu ya kupata sadaka za wanyama, wanyama wengi walikuwa wakiuzwa na kununuliwa hapo katika uwanja wa nje wa hekalu.TVV 80.2

    Kila mwaka, Myahudi alitakiwa kutoa sadaka kwa ajili ya roho yake. Fedha zilikusanywa kutengeneza hekalu. Soma Kutoka 30:1,2-16. Zaidi ya fedha hizi, jumla kubwa ya fedha zililetwa kama mchango, na kutiwa katika hazina. Uvunjaji wa fedha hizo uliimarisha udanganyifu na utozaji gharama isiokuwa halali, ambao ulihesabiwa kuwa ni fungu la makuhani.TVV 80.3

    Wenye kuabudu walifundishwa kuwa, wasipotoa fedha hizo kama sadaka, mibaraka ya Mungu haitawakalia katika ibada yao na wala nchi yao haitabarikiwa pia. Wenye biashara waliuza wanyama wao kwa bei ya juu sana, na faida wakagawana na makuhani na wakuu wengine. Hivyo walijitajirisha kwa ajili ya kuwatoza watu bure.TVV 80.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents