Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    12 — Majaribu

    “Ndipo Yesu alipoongozwa na Roho mpaka jangwani, ili apate kujaribiwa na shetani. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, baadaye aliona njaa.”TVV 56.1

    Yesu hakujitia majaribuni mwenyewe. Alikwenda jangwani ili akae peke yake, apate kutafakari juu ya kazi yake Alikuwa akijifikiria na kujikaza kuhusu njia ngumu ya hatari, ambayo ataiendea. Lakini Shetani alidhani kuwa huo ndio wakati mzuri wa kumkabili.TVV 56.2

    Matokeo makubwa yalikuwa hatarini. Shetani alidai kuwa dunia hii ni mali yake, na yeye mwenyewe hujiita “Mtawala wa ulimwengu.” Husema kuwa watu wamemchagua awe mtawala wao. Kwa ajili hiyo amepata utawala wa ulimwengu. Kristo alikuja ili kuyakanusha madai hayo. Kristo atadumu kuwa mwaminifu kwa Mungu, akiwa katika hali ya binadamu. Hivyo itaonyesha kuwa Shetani hakuutawala ulimwengu kamili, na madal yake kuwa ni mfalme wa ulimwengu, ni uongo. Wote wanaotamani kutolewa mikononi mwake watafunguliwa.TVV 56.3

    Shetani aliiua kuwa hakuutawala ulimwengu kamili. Ulionekana uwezo katika wanadamu unaoupinga utawala wake. Soma Mwanzo 3:15. Katika kafara iliyotolewa na Adamu na wazao wake, ilionekana alama ya kuongea kati ya dunia na mbingu. Shetani alijitia kati kuzuia mawasiliano haya. Alimtaja Mungu vibaya na kueleza kinyume juu ya mifano iliyokuwa ikimwelekeza mwokozi. Watu walimwogopa Mungu kama mwenye kufurahia maangamizi yao. Kafara ambazo zingalionyesha upendo wake, zilipotoshwa na kufanya kuwa kumfurahisha Mungu ili awahurumie. Sura hii imeandikwa katika Mathayo 4:1-ll; Marko 1:12, 13; Luka 4:1-13, Wakati Neno la Mungu lilipotolewa, Shetani alijifunza unabii. Toka kizazi mpaka kizazi, alijitahidi kuwapofusha watu ili wamkane Kristo na kuja kwake.TVV 56.4

    Wakati wa kuzaliwa kwa Kristo, Shetani alijua kuwa amekuja atakayepinga utawala wake. Kwamba Mwana wa Mungu angekuja ulimwenguni kama mtu mwenye uwezo wa kukamata na kuangamiza. Roho yake ya ubinafsi isingeweza kufahamu upendo huo. Kwa kuwa mwenyewe amekosa kuishi mbinguni, aliazimia kuwapotosha wengine, ili washiriki ajali yake. Alitaka kuwafanya watu wadharau mambo ya mbinguni, ila wathamini mambo ya dunia tu.TVV 57.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents