Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    51 — Nuru ya Uzima

    “Mimi ni nuru ya ulimwengu: Anifuataye hataenda gizani, bali atakuwa na nuru ya uzima.”TVV 263.1

    Ilikuwa asubuhi, jua lilikuwa limepanda juu ya mlima wa mizeituni, na miangaza yake ilikuwa iking’aa kwenye hekalu lenye mawe ya thamani, kuta za dhahabu, ndipo Yesu aliposema, ‘Mimi ni nuru ya ulimwengu.” Maneno haya baadaye yalisemwa na Mtume Yohana kama hivi: ‘Ndani yake ulikuwamo uzima, na uzima ulikuwa nuru ya watu. Nuru iling’aa gizani wala giza halikuiweza.” “Nuru ya kweli imwangazaye kila mtu ajaye ulimwenguni.” Yohana 1:4, 5, 9. Mungu ni nuru; na katika maneno yale yasemayo kwamba: “Mimi ni nuru ya ulimwengu”, Kristo husema kuhusu umoja wake na Mungu na uhusiano wake na ubinadamu. Ni yeye ambaye mwanzoni alifanya “nuru ing’ae gizani.” 2 Kor. 4:6. Yesu nuru ya jua, na mwezi na nyota. Jinsi mishale ya jua inavyopenya katika pande zote za nchi, ndivyo ilivyo kwa jua la haki linavyong”aa kwa kila mtu.TVV 263.2

    “Hiyo ilikuwa nuru halisi iliyomulikia kila mtu ajaye ulimwenguni.” Watu hodari, wenye uwezo mkubwa na akili nyingi sana ndio waliofungua fani mbalimbali za elimu, na uvumbuzi mwingi. Lakini mmoja huwapita wote. “Wote wale waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika wana wa Mungu ” “Hakuna mtu aliyemwona Mungu, Mwana pekee, aliye katika kifua cha Baba ndiye alimwona.” Yohana 1:12,18.TVV 263.3

    Tunaweza kufuata walimu wakuu wa uliwengu kwa kadiri ya kumbukumbu za watu zilivyo; lakini nuru ilikuwa kabla yao. Jinsi mwezi na nyota zinavyorudisha nuru ya jua, hali kadhalika walimu wakuu wa dunia kadiri ilivyo kweli hurudisha tu elimu ya jua la haki, yaani Yesu Kristo. Elimu ya kweli hutolewa naye, ambaye, ‘Ndani yake zimesitirika hazina zote za maarifa yote.” Wakolosai 2:3. ‘Anifuataye hatakwenda gizani, bali atakuwa na nuru ya uzima.”TVV 263.4

    Wakati Yesu aliposema kuwa, ‘Mmi ni nuru ya ulimwengu”, watu walifahamu kwamba ndiye Masihi aliyeahidiwa. Mafarisayo na wakuu waliona kuwa hayo ni majivuno. Waliona kuwa kwa mtu kama wao kusema hivyo haiwezekani kumvumilia zaidi. Wakasema: “Wewe ni nani?” Walitaka awaambie kama yeye ni Kristo. Adui zake waliamini kuwa hali yake na kazi yake zilikuwa tofauti na tazamio la watu kiasi kwamba akiwaambia hivyo, angalikataliwa na watu kuwa ni mlaghai.”TVV 264.1

    Lakini Yesu alijibu: “Hata nilivyowaambieni tangu mwanzo, ndivyo.” Alikuwa mfano halisi wa ukweli aliofundisha. “Mimi sifanyi neno kwa shauri langu, ila nasema yale niliyofundishwa na Baba. Naye aliyenituma yu pamoja nami.” Hakutaka kuthibitisha kwamba yeye ni Masihi, ila alionyesha kwamba yu umoja na Baba yake, Mungu. Kati ya wasikilizaji wake, wengi walimwamini. Kwa hiyo aliwaambia: “Mkishika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli, nanyi mtaifahamu kweli, na kweli itawaweka huru.”TVV 264.2

    Maneno hayo yaliwachukiza Mafarisayo wakasema: “Sisi tu wana wa Ibrahim wala hatujawa watumwa wakati wowote, wasemaje kuwa mtakuwa huru?” Yesu akawaangalia watu hawa wakiwa watumwa wa uovu, akasema kwa masikitiko: “Amin nawaambieni yeye atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.’ Walikuwa katika dhambi mbaya sana, wakitawaliwa na roho ya mwovu.TVV 264.3

    Kila mtu anayekataa kujitoa kwa Mungu, hutawaliwa na nguvu nyingine. Huwa katika utumwa mbaya sana, akili zake huongozwa na Shetani, Kristo alikuja kuzivunja nguvu za Shetani. “Kama Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.”TVV 264.4

    Katika kazi ya ukombozi hakuna lazima. Mtu hawezi kushurutishwa kuamini. Kila mtu huachwa achague atakayemtumikia kwa hiari yake. Mtu anapojitoa kwa Kristo huwa na uhuru kamili wa kuchagua. Kukataa dhambi ni kazi ya roho ya mtu. Tunapotamani kuwekwa huru mbali na dhambi, na tunapolia ili tupewe uwezo kutoka juu ili utuwezeshe, moyo hujazwa uwezo wa Roho Mtakaifu, ili uweze kutii maongozi ya Roho Mtakatifu ambayo ndiyo mapenzi ya Mungu.TVV 264.5

    Sharti moja tu la kuwezesha uhuru wa mwanadamu kukamilika ni kule kuambatana na Yesu, yaani umoja na Kristo. Dhambi hufaulu tu, umoja huo unapoharibika. Kujitoa kwa Mungu kikamihfu ndiyo heshima ya binadamu. Sheria ya Mungu ambayo ndiyo inayotuleta kwa Mungu ni ‘sheria ya uhuru”. Yak. 2:12.TVV 264.6

    Mafarisayo walijitaja kuwa ni wana wa Ibrahim. Wana wa kweli hawawezi kujaribu kuua mtu ambaye hunena kweli itokayo kwa Mungu. Kule kuwa wazao wa Ibrahim tu hakuna thamani yoyote. Pasipokuwa na nia ya Ibrahim na, kutenda matendo ya Ibrahim hawawezi kuwa wana wa Ibrahim.TVV 265.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents