Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  18 — Yeye Hana Budi Kuzidi Bali Mimi Kupungua’

  Kama Yohana Mbatizaji angalijitangaza mwenyewe kuwa ni yeye Masihi, na afanye upinzani kwa senkali ya Kirumi, makuhani na watu wangalimfuata. Kila aina ya upinzani na kutaka heshima ya dunia hii, Shetani huunga mkono. Lakini Yohana alikataa kabisa heshima hiyo. Heshima iliyomwelekea, yeye aliielekeza kwa mwingine.TVV 94.1

  Sasa aliona makundi ya watu yakigeuka kutoka kwake na kumwelekea Mwokozi. Kila siku kundi la watu waliomjia lilizidi kupungua, maana walikwenda kumsikiliza Yesu. Jumla ya watu waliomfuata Yesu walizidi kuongezeka kila siku.TVV 94.2

  Lakini wanafunzi wa Yohana waliangalia jambo hilo kwa wivu. Wakawa tayari kumlaumu Yesu, na kazi yake. Mara swali likatokea baina ya wanafunzi wa Yohana na makuhani, kuhusu ubatizo, kwamba ubatizo hutakasa moyo wa mtu kutokana na dhambi. Walisema kuwa ubatizo wa Yesu unatofautiana na wa Yohana. Mara yakatokea mabishano kati ya wanafunzi wa Yesu na wa Yohana, kuhusu maneno yafaayo kutumiwa wakati wa ubatizo; na haki yao ya kubatiza watu. Wanafunzi wa Yohana walimjia wakiwa na masikitiko, wakisema: “Mwalimu, yule mliyekuwa naye huko Yordani, ambaye alisikia sauti ya uthibitisho, anabatiza watu pia, na watu wote wanamfuata.”TVV 94.3

  Kwa maneno haya, Shetani alileta jaribu kwa Yohana. Kama Yohana angalilalamika kwa kuwa amedharauliwa, na kuingiliwa, angekuwa amepanda mbegu za fitina, za mashaka na za wivu, katikati ya maendeleo ya Injili.TVV 94.4

  Yohana alikuwa na upungufu na kasoro za kibinadamu kama kawaida ya wote. Lakini upendo wa Mungu umembadilisha. Alikuwa katika hali ambayo si rahisi kuchafuliwa na ubinafsi, na tamaa kutaka makuu. Hakuonyesha hali ya kukubaliana na wanafunzi wake, ila alionyesha kuwa alimfurahia yule ambaye yeye anamtengenezea njia.TVV 94.5

  Alisema: “Hakuna mtu apokeaye kitu, isipokuwa amepata kutoka mbinguni. Ninyi wenyewe mnanishuhudia kuwa nimesema kuwa mimi siye Kristo, ila nimemtangulia. Aliye na bibi arusi ndiye Bwana arusi, rafiki wa bwana arusi, anayesimama karibu naye na kumsikiliza, huifurahia sana sauti yake.” Yohana huwakilisha kama rafiki anayetumwa kati ya watu wawili wonaochumbiana; wakijitayarisha kwa ndoa. Bwana arusi anapokwisha kumpokea Bibi arusi, kazi ya rafiki, au msindikizaji, huwa imetimilika. Hufurahia katika shangwe ya maarusi. Ndivyo ilikuwa kwa Yohana pia kushuhudia jinsi kazi ya Mwokozi inavyofaulu. Kwa hiyo alisema: “Shangwe yangu imetimilika. Lazima azidi, na mimi nipungue.”TVV 95.1

  Akimwangalia Mwokozi kwa njia ya imani, Yohana alikuwa ameinuka juu ya kujikana nafsi. Yeye alikuwa ni sauti tu, iliayo nyikani. Na sasa anafurahi kukaa kimya, ili macho ya watu wote yaelekee kwenye Nuru ya uzima.TVV 95.2

  Moyo wa nabii Yohana usiokuwa na kiburi wala majivuno, ulijazwa na mwanga wa Mungu. Kwa hiyo alisema: “Ashukaye kutoka juu, yu juu ya yote .... Maana aliyetumwa na Mungu hunena maneno ya Mungu, maana Mungu hampi Roho ya kumpima, ila humpa tele.” Kristo aliweza kusema: “Sitafuti kufanya mapenzi yangu mwenyewe, bali mapenzi ya Baba aliyenituma.” Yohana 5:30.TVV 95.3

  Vivyo hivyo na wafuasi wa Kristo. Tunaweza kupokea nuru ya mbinguni tu, tunapokuwa tayari kuondoa ubinafsi ndani yetu, na kukubali kuleta kila wazo limtii Kristo. Wote wafanyao hivyo, Roho Mtakatifu hutolewa kwao bila kipimo.TVV 95.4

  Kufaulu kwa kazi ya Kristo, ambayo Yohana alikuwa akiifurahia, ilijulikana hata kwa wakuu huko Yerusalemi. Makuhani na walimu wakuu, yaani marabi, walikuwa na wivu kwa maendeleo ya Yohana, kwa vile walivyoona watu wengi wakitoka katika masinagogi na kwenda jangwani kwa Yohana. Lakini sasa yuko mwenye uwezo mkuu anayewavuta watu wengi kumwendea. Waongozi wa Waisraeli hawakuwa tayari kusema kwa Yohana kwamba, “lazima azidi, na mimi nipungue.”TVV 95.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents