Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    61 — Mtu Mfupi Aliyekuwa Mashuhuri

    Mji wa Yeriko ulijengwa katika uwanda wa katikati katika Tropiki, mahali pazuri sana penye majani mazuri, na kuzungukwa na chemchemi za maji na vilima vinavyong’aa kama chokaa. Mji ulikuwa kituo kikuu cha biashara. Wakuu wa Kirumi na askari; pamoja na wageni wengi kutoka kila mahali walipatikana hapa. Watoza kodi wengi walikuwa wanashughulika kutoza ushuru.TVV 308.1

    Mkuu wa watoza ushuru alikuwa Myahudi aitwaye Zakayo, alikuwa akichukiwa sana na watu wa kwao kwa kumfikiria alijitajirisha kwa njia za dhuluma. Walakini hata hivyo Zakayo hakuwa kama vile watu walivyomdhani. Zakayo alikuwa amemsikia Yesu. Habari za wema wake na fadhili zake kwa watu wote zilienea kila mahali. Yohana Mbatizaji alikuwa amehubiri Yordani na Zakayo alikuwa amesikia mwito wa kutubu. Na sasa aliposikia habari za Mwalimu Mkuu, alijiona kuwa mwenye dhambi mbele za Mungu. Walakini habari za Yesu alizosikia zilimchangamsha moyo.TVV 308.2

    Akaona kuwa ana haja ya kutubu na kujirekebisha. Je, mtoza ushuru mwingine hakuwa mfuasi mwaminifu wa Mwalimu, ingawa ni mtoza ushuru? Zakayo alianza kufanya mipango ya kutekeleza mchangamko wake. Habari ilipotangazwa kwamba Yesu anaingia Yeriko, Zakayo aliazimu kumwona.TVV 308.3

    Mtoza ushuru huyu alitamani kuona uso wa mtu mwenye maneno yaliyomletea tumaini moyoni mwake.TVV 308.4

    Njia zilikuwa zimejaa watu, na Zakayo ambaye alikuwa mtu mdogo na mfupi hangeweza kuona chochote kwenye watu warefu jinsi hiyo. Kwa hiyo Zakayo alitangulia mbele, akapanda juu ya mkuyu. Wakati mkutano ulipopita alikodoa macho yake kwa hamu ili apate kuona sura ya mtu huyu aliyemtamani.TVV 308.5

    Ghafla mkutano ulisimama chini ya mkuyu huo. Mtu ambaye aliweza kusoma mioyo ya watu, alitazama juu. Mtu huyu aliyekuwa juu ya mkuyu alisikia sauti ya mtu ikisema: “Zakayo, shuka upesi, kwa maana leo nitashinda nyumbani kwako.”TVV 309.1

    Zakayo alishuka. Akitembea kama mtu yumo ndotoni aliongoza njia kwenda nyumbani kwake. Lakini marabi na watu wengine katika mkutano walinung’unika wakisema, Anakwenda kwa mtu mwenye dhambi.TVV 309.2

    Zakayo alikuwa na wasiwasi mwingi sana kwa Yesu kuingia kwake, maana alijiona kuwa hastahili hata kidogo. Sasa upendo kwa Bwana wake mpya na mgeni wake, ulimfanya asinyamaze. Ataungama wasiwasi mbele ya watu. Zakayo alisimama mbele ya mkutano akasema: “Bwana, tazama, nusu ya mali yangu nitawagawia maskini, na ikiwa kuna mtu yeyote niliyemdhulumu, nitamrudishia mara nne. Yesu akasema: “Leo wokovu umeingia nyumbani humu, kwa kuwa huyu naye ni mtoto wa Ibrahim.”TVV 309.3

    Sasa wanafunzi walionyeshwa kielelezo dhahiri cha maneno ya Kristo jinsi yalivyo kweli kwamba; “Yasiyowezekana kwa wanadamu yawezekana kwa Mungu yawezekana” Luka 18:27. Waliona sasa kwa uwezo wa Mungu kwa tajiri anaweza kuingia ufalme wa Mungu.TVV 309.4

    Kabla Zakayo hajamwangalia Bwana uso wake, aliungama kwanza dhambi zake. Alianza kutekeleza maandiko yaliyoandikwa zamani, kwamba, “Ndugu yako akiwa maskini, na akawa hawezi kujisaidia, msaidie, awe kama mgeni au msafiri kwako. Usimtoze faida ya kitu chochote ila mche Mungu.”TVV 309.5

    “Msitendeane ubaya ninyi kwa ninyi, bali mtamcha Mungu wenu, kwa maana mimi ni Bwana Mungu wenu.” Mambo ya Walawi 25:35, 36, 17. Jambo la kwanza Zakayo alilosema kwa Kristo, kuonyesha toba yake lilikuwa kuwafadhili maskini na wenye dhiki. Kati ya watoza ushuru kulikuwa na umoja wa kuwadhulumu watu, na kusaidiana wao kwa wao. Lakini Zakayo alipoamini alitupilia mbali matendo yasiyokuwa ya adili.TVV 309.6

    Hakuna maungamo yaliyokamlika, isipokuwa yawe na matengenezo ya mambo yaliyokwenda upogo. Haki ya Kristo siyo koti la kuficha dhambi ambazo haziachi kutendwa na mtu. Utakatifu ni hali ya kutakaswa kwa Mungu, kwa njia ya kujitoa kamili kwake, na kufuatana na kanuni za mbinguni.TVV 309.7

    Mkristo katika shughuli zake ulimwenguni ni kumdhihirisha Kristo na kuonyesha namna ambayo. Kristo mwenyewe angekuwa. Kwa kila tendo atendalo angeonyesha kuwa Mungu ndiye mwalimu wake. Neno: “Utakatifu kwa Bwana” lingeandikwa katika mambo yake yote atendayo. Kila muumini wa Kristo angeonyesha kuwa anaruhusu utakatifu umkalie, kwa njia ya kuachana na matendo yote yasiyokuwa ya kweli. Ataonyesha ukweli wake waziwazi kama Zakayo alivyofanya. Maandiko husema: “Kama mwovu akirudisha amana yake, na kumrudishia mtu mali aliyomwibia na kutembea katika njia ya haki, bila kutenda maovu ataishi hakika.” Ezeldeli 33:15.TVV 309.8

    Kama tumewaumiza wengine, tumedanganya katika biashara, au tumemdhulumu mtu yeyote, hata kama tumeasi sheria yoyote, tutaungama dhambi zetu, na kufanya matengenezo na kurekebisha mambo yetu, kwa kadiri ya uwezo wetu. Si lazima turudishe vitu tulivyodhulumu tu, lakini hata vyote ambavyo havikutumika.TVV 310.1

    Mwokozi alisema kwa Zakayo: “Leo wokovu umeingia katika nyumba hii.” Kristo alikwenda kwa Zakayo kumfundisha ukweli, na kufundisha nyumba yake mambo ya ufalme wa mbinguni. Waliokuwa wametengwa na marabi wasiingie katika masinagogi, sasa walikusanyika nyumbani wakiwa na mwalimu wa mbinguni, ili kusikia neno la uzima.TVV 310.2

    Kristo anapopokelewa kama Mwokozi wa pekee, wokovu huja kwa yule aliyempokea. Zakayo alimpokea Yesu si kama mgeni mpitaji, ila kama mgeni wa kudumu katika moyo siku zote. Waandishi na Mafarisayo walimshutumu kama mtu mwenye dhambi, lakini Mwokozi alimtambua kuwa kama mwana wa Ibrahim. Wagalatia 3:7, 29.TVV 310.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents