Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    42 — Kristo Atabiri Juu ya Maanguko

    Kazi ya wale mitume kumi na wawili ikiongezeka na kupanuka kwa kazi ya Yesu ilileta mwamko mpya wa wivu kwa waongozi wa Yerusalemu. Makuhani waliotumwa Kapernaumu hapo mapema mwanzoni mwa kazi ya Kristo, walitatanika vikubwa, lakini sasa wajumbe wengine walipelekwa huko ili kuchungua mwenedo wake na kazi yake wapate cha kumshitakia.TVV 219.1

    Kama ilivyokuwa hapo kwanza, ni kwamba makosa yake ni ya kutojali kushika mapokeo waliyofundishwa yanayolinda sheria. Kati ya mapokeo muhimu ambayo Yesu hakuyajali yalihusu sheria ya kawaida inayoelekeza kuja kwa Masihi, ambayo itafutika akija na kutimiza yote. Kutofuata sheria ya kunawa mikono kabla ya kula ilihesabiwa kuwa ni dhambi mbaya sana.TVV 219.2

    Maisha ya wale walioishika sheria ya Marabi, yalikuwa maisha ya matatizo matupu. Watu walipokuwa wakishughulika na kushika sheria hizo, maisha yao yalikuwa mbali sana na kanuni za sheria za Mungu.TVV 219.3

    Kristo na wanafunzi wake hawakuzijali sheria hizo za kunawa. Wale wapelelezi waliotumwa hawakuweza kumshambulia Yesu wazi, ila walipitia kwa njia ya wanafunzi wake. Walisema: “kwa nini wanafunzi wako wanavunja sheria za wazee? maana hula bila kunawa mikono yao.”TVV 219.4

    Yesu hakujaribu kujitetea au kutetea wanafunzi wake. Aliwaonyesha tu, maana ya sheria hizo. Aliwapa mfano wa kuzikariri kwao; alisema: “ninyi mnaacha sheria ya Mungu, ilimshike sheria ya wanadamu. Maana Musa alisema Mheshimu baba yako na mama yako; amlaaniye baba yake au mama yake, na afe; lakini ninyi husema, mtu asemaye kwa babaye au kwa mamaye kuwa, mali hii ni wakfu, wala asimsaidie baba au mama, atakuwa huru, asimsaidie baba au mama mtu kutamka kuwa mali yake ni wakfu, wala isitumike siku zote za maisha yake, na akifa isitumike hekaluni, huko ni kumdhulumu babaye na mamaye, huku wakijisingizia kuwa ni wakfu.TVV 219.5

    Yesu alimsifu mjane maskini aliyetoa vyote kwa hekalu kuwa sadaka. Juhudi kubwa ya makuhani na marabi kwa kazi ya Mungu na uchaji wao, ilikuwa ni kujionyesha kwa nje kwamba wao ni watakatifu na watawa kamili. Hata wanafunzi wa Yesu pia hawakuachana kamili na hali ya mafarisayo na marabi. Yesu alijitahidi kuwaondolea hali hiyo mbaya watu wote wanaofanya kazi ya Mungu.TVV 220.1

    “Ninyi manafiki, ni vema Isaya alivyowatabiria ninyi akisema, “Watu hawa huniheshimu kwa vinywa vyao, na kwa midomo yao hufanya mapenzi mengi; lakini mioyo iko mbali nami. Nao huniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.” Kristo alisema kuwa kuweka maagizo yao yawe juu ya amri za Mungu, marabi walikuwa wakijitukuza juu ya Mungu, marabi walikuwa wakijitukuza juu ya Mungu, yesu alitamka kwamba unajisi hautokani na mambo ya nje, bali hutokana na mambo ya ndani. Usafi au uchafu hutoka moyoni.TVV 220.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents