Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  57 — Kijana Tajiri Mtawala Amepungukiwa na jambo Moja

  “Alipokuwa njiani akienda mtu mmoja alimjia akikimbia, akamwuliza akisema: “Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?” Mtu huyu mtawala, alikuwa na mali nyingi na madaraka makubwa. Aliona upendo Yesu aliokuwa nao kwa watoto. Moyo wake uliwaka kwa ajili ya Mwokozi. Alivutiwa mno kiasi cha kumkimbilia Yesu, na kumpigia magoti kwa nia hasa, na kuuliza swali muhimu kwake na kwa watu wote.TVV 292.1

  Kristo alisema: “Kwa nini kuniita mwema?’ Hakuna mwema, ila mmoja tu ndiye Mungu.’ Je, alifahamu kuwa yule aliyekuwa akizungumza naye ndiye Mwana wa Mungu? Elezo lake lilikuwa la kweli kiasi gani?TVV 292.2

  Mtawala huyu alikuwa akijiona kuwa yu mwenye haki kabisa, walakini alijisikia kuwa hana kitu kimoja. Je, inawezekana Yesu kumbariki na kuuridhisha moyo wake? Katika majibu ya Yesu alimwambia kuwa utii kwa amri za Mungu ni lazima, kama mtu akitaka kuurithi uzima wa milele. Jibu la kijana huyu lilikuwa dhahiri. Alisema: “Yote hayo nimeyashika tangu utoto wangu, nimepungukiwa nini tena?”TVV 292.3

  Kristo alimtazama usoni, kama mtu anayesoma habari za maisha yake, na kuchunguza tabia yake. Alimpenda na akatamani kumpatia amani na furaha. , Alimwambia: “Umepungukiwa na kitu kimoja, nenda ukauze vyote ulivyo navyo, ukawape maskini nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha njoo ujitwike msalaba wako unifuate.”TVV 292.4

  Kristo alivutiwa sana na kijana huyu. Mwokozi alitamani kumfunulia ibada halisi ya moyo. Alitamani kumwona akijinyenyekeza kikweli bila kujificha na kujifanya kwamba anashika dini ya kweli.TVV 292.5

  Yesu alirnwona mtu huyu kuwa anahitaji, msaada unaohusu wokovu. Kama akijitoa kamili kwa Kristo atakuwa mwenye uwezo wa kutenda mema. Alipochungulia tabia yake alimpenda. Upendo wa Kristo ulimwamsha, akatamani kuwa mtu v ake. Yesu pia alitamani kumwongoa, na kuendeleza tabia yake hiyo bora, ipate kuwa katika utumishi wa Bwana. Kama mtu huyu angalijitolea kwa Kristo, angalibadilika kadiri gani siku za usoni!TVV 292.6

  Yesu alisema: “Umepungukiwa na kitu kimoja.” Nenda ukauze vitu ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha njoo unifuate.” Kristo aliona moyo wake. Alipungukiwa na kitu kimoja tu, ni hicho kilikuwa sharti kubwa lenye kanuni. Alihitaji upendo wa Mungu moyoni mwake. Jambo hili ndilo alilopungukiwa, na lisipopatikana atakuwa ameshindwa kabisa. Maisha yake yote ya usoni yatakuwa yameharibika kabisa. Ili kusudi apokee upendo wa Mungu, lazima upendo wa ubinafsi uachwe kabisa.TVV 293.1

  Kristo alimwambia achague kati ya hazina ya mbinguni na hazina ya duniani, na ukubwa wake. Ubinafsi lazima utupiliwe mbali, na mapenzi yake lazima yatolewe yote kwa Kristo. Kijana huyu alikuwa na bahati ya kuchagua hazina za mbinguni na kurithi pamoja na Kristo. Lakini hana budi kuchukua msalaba na kumfuata Yesu katika njia ya kujikana nafsi.TVV 293.2

  Uchaguzi uliachwa juu yake. Yesu alikuwa amemwonyesha maana ya amri kumi anazosema kuwa ameshika tangu utoto wake. Akitaka kumfuata Kristo, lazima akubali kuacha matazamio yake ya siku za usoni. Yesu alimtazama kijana huyu kwa makini, akitumaini kuwa atakubali kufuata njia ya Mungu ya kujikana nafsi, kama anavyoshauriwa na Roho Mtakatifu.TVV 293.3

  Maneno ya Kristo yalikuwa maneno ya hekima, na ijapokuwa yalionekana kana kwamba ni makali. Kuyakubali na kuyafuata, ndilo lilikuwa tumaini la mtu huyu la kupata wokovu. Cheo chake na mali zake vilikuwa vikibashiri mabaya tu, katika tabia yake. Kama vikiendekezwa vitamfukuza Mungu katika mawazo yake.TVV 293.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents