Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mwimbaji Mchangamfu

  Kila mara Yesu alionyesha furaha ya moyo wake kwa njia ya kuimba Zaburi, na nyimbo nyingine za mbinguni. Mara kwa mara wenyeji wa Nazareti walimsikia akiimba nyimbo za sifa. Wenzake walipo kuwa wakilalamika kwa sababu ya kuchoka, walichangamshwa kwa nyimbo alizoimba.TVV 35.4

  Kwa miaka yote aliyokaa Nazareti, maisha yake yalikuwa ya kusaidia na kufariji wengine. Alisaidia wazee, wenye huzuni, wenye kulemewa na dhambi, watoto katika michezo yao, viumbe vidogo vidogo, wanyama wenye taabu. Kila mara wote walimfurahia popote anapokuwa. Anayeusimamisha ulimwengu, alishuka chini kumhudumia ndege aliyeumia. Hakuna kitu kilichopitwa bila kuhudumiwa.TVV 36.1

  Hivyo ndivyo alivyokuwa mwenye hekima., na kimo akimpendeza Mungu na watu pia. Alijionyesha kuwa mwenye huruma kwa wote. Hali yake na mahali pake, vilikuwa mibaraka ya wote. Mara kwa mara siku ya sabato aliitwa kusoma maneno ya manabii, na watu walifurahia mambo hayo sana.TVV 36.2

  Walakini katika muda huo wote wa kuishi Nazareti, hakutenda tendo lolote la mwujiza, wala hakuwa na cheo chochote. Maisha yake ya utulivu yalifundisha fundisho la maana sana. Maisha ya kutoiga mambo ya kubuni, na ya ovyo huwa na maana sana kwa watoto, na kuchunguza viumbe vya Mungu hupanua mawazo zaidi.TVV 36.3

  Yesu ni kielelezo chetu. Katika maisha ya nyumbani ndiye wa kuigwa na watoto wote na vijana. Mwokozi aliwatendea maskini wema kabisa, ili kutuonyesha jinsi ya kutembea pamoja na Mungu. Kazi yake ilianzia na uaminifu katika kazi za nyumbani, fundi anayeshughulika ili apate chakula.TVV 36.4

  Wakati alipokuwa akifanya kazi ya useremala, alikuwa akifanya kazi ya Mungu hasa, sawa kama angejishughulisha kuwahudumia makutano. Kila kijana anayefuata kielelezo cha Yesu, cha kuwa mwaminifu na mtiifu, na mpole katika maisha ya nyumbani, atahusika na maneno haya: “Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye, mteule wangu, ambaye nafsi yangu yapendezwa naye.” Isaya 42:1.TVV 36.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents