Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mbinguni Kanuni hii ilivunjika!

  Dhambi ilianza katika ubinafsi. Lusifa, ambaye ni Kerubi wa kusitiri, alitamani kuwa wa kwanza mbinguni. Alitafuta kuwavuta viumbe wote wa mbinguni wamwache Muumba wao, akajitafutia heshima yake mwenyewe. Alimtupia Muumbaji malaumu maovu kwa uongo, aliwatatanisha malaika na kuwatia mashakani juu ya neno la Mungu. Wakaanza kuona mashaka kuhusu wema wa Mungu. Shetani akawashawishi wamheshimu Mungu kuwa ni mkatili asiye na huruma, wala hasamehi. Kwa njia hiyo aliwadanganya malaika. Kwa njia hiyo aliwadanganya wamdamu pia. Hivyo giza likaufunika ulimwengu.TVV 10.2

  Ulimwengu ulikaa gizani kwa kutomwelewa Mungu na tabia yake. Ili kurudisha ulimwengu kwa Mungu ilipasa nguvu ya Shetani ya kudanganya ivunjwe. Jambo hili lisingetendwa kwa kutumia nguvu. Mungu alitaka huduma ya upendo tu, na upendo usingepatikana kwa kutumia nguvu na uwezo. Upendo tu, ndiyo utawaamsha watu. Kumjua Mungu ni kumpenda. Tabia yake lazima ipambanuliwe na ile ya Shetani. Yule ajuaye urefu na kina cha upendo wa Mungu ndiye tu anaweza kufanya hivyo.TVV 10.3

  Mpango wa wokovu wetu haukuanzwa wakati ule Adamu alipoanguka dhambini. Ulikuwa mafunuo ya siri iliyofichika tangu zama za milele. Warumi 16:25. Ilikuwa ni ufunuo wa nambo Yaliyofichika kale na kale katika kiti cha enzi cha Mungu. Mungu aliiona dhambi ikitokea, naye akafanya matayarisho ya kuikabili dhambi hiyo. Aliahidi kumtoa mwana wake wa Pekee. Yohana 3:16.TVV 10.4

  Lusifa alikuwa amesema, “Nitapandisha kiti changu juu kupita nyota za Mungu . . . Nitafanana naye aliye juu”. Lakini Kristo ambaye ni sura ya Mungu alijitoa mwenyewe, akatwaa umbo la mwanadamu ambaye ni mtumwa, akiwa na umbo la mwanadamu akajinyenyekeza mpaka kufa, naam kifo cha msalaba.” Isaya 14:1, 3, 14; Wafilipi 2:6, 7.TVV 10.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents