Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    79 — Jinsi Kifo Cha Kristo Kilivyomshinda Shetani

    Kristo alikuwa ametimiza kazi aliyokuja kuifanya na kwa pumzi yake ya mwisho akasema kwa sauti kuu “Imekwisha.” Yohana 19:30. Alikuwa ameshinda vita. Mbingu yote ilishangilia kwa ushindi wa Mwokozi. Shetani alijua kuwa utawala wake umekwisha. Ilikuwa ni kwa ajili ya malaika, sayari ambazo hazikuanguka na kwa ajili yetu pia kwamba kazi kubwa ya ukombozi ilikuwa imekamilishwa. Hadi ya kifo cha Kristo, Shetani alikuwa amejificha kabisa asijulikane jinsi alivyo, hata malaika watakatifu hawakufahamu kanuni zake wala kuona kwa wazi asili ya uasi wake. Lusifa alikuwa kerubi wa kusitiri, mwenye hadhi ya juu kuliko viumbe vyote. Alikuwa msitari wa mbele katika kuelezea makusudi ya Mungu katika ulimwengu. Baada ya kufanya dhambi uwezo wake wa kudanganya ulikuwa mwerevu mno na kugundua tabia yake ilikuwa vigumu zaidi kwa sababu ya utukufu aliokuwa nao pamoja na Baba hapo awali.TVV 430.1

    Mungu angeweza kumwangamiza Shetani na malaika waliomuunga mkono, lakini hakufanya hivyo. Kutumia nguvu na kulazimisha hupatikana tu chini ya serikali ya Shetani. Utawala wa Mungu umejengwa katika wema, rehema, upendo, na kanuni hizi ndizo zinazotumika. Serikali ya Mungu ni adilifu, na kweli na upendo, ndizo kanuni za mamlaka yake. Katika baraza la mbinguni iliamriwa kuwa lazima muda utolewe kwa Shetani kuweza kudhihirisha kanuni za utawala wake waziwazi. Maana alikuwa amedai kuwa utawala wake ulikuwa bora zaidi kuliko wa Mungu. Muda ulitolewa kwa kanuni za Shetani kutenda kazi, kusudi wakazi wa mbinguni wapate fursa ya kuona matokeo ya utawala wake. Kwa muda wa miaka 4,000 Kristo alikuwa akifanya kazi ya kumwinua mwanadamu na Shetani akidhamiria kumwangamiza. Walioko mbinguni walikuwa wakiyaangalia hayo.TVV 430.2

    Tangu wakati ule Yesu alipoonekana kama mtoto huko Bethlehemu, Shetani alijitahidi kumwangamiza. Alitafuta njia ya kumzuia asiendeleze tabia njema akiwa mtoto, mtu mzima mkamilifu huduma takatifu, na kafara isiyo na mawaa. Lakini Shetani alishindwa. Hakuweza kumshawishi Yesu afanye dhambi. Juhudi zote za Shetani dhidi ya Yesu zilidhihirisha kwa nuru ya wazi tabia isiyokuwa na kasoro.TVV 430.3

    Kwa hamu kuu wakaaji wa mbinguni na wa sayari zingine ambazo hazikuanguka waliangalia hatua za mwisho za hili pambano kuu. Walisikia kilio chake cha uchungu, “Baba, yangu ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke.” Mathayo 26:39. Walimwona akihuzunika kwa uchungu uliopita pambano la mwisho dhidi ya mauti. Jasho la damu, lililazimika kuchuruzika usoni na mara tatu ombi la kuokolewa lilimtoka. Mbingu zilishindwa kuendelea kuvumilia hali hiyo na mjumbe alitumwa kuja kumfariji, Mwana wa Mungu.TVV 431.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents