Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ndugu halisi wa Kristo

    Yesu alipokuwa akiwafundisha watu, wanafunzi wake walileta habari kwamba, mama yake na ndugu zake walikuwa huko nje, wakitaka kumwona. Lakini alimjibu mtu yule aliyempa habari: Mama yangu ni nani, na ndugu zangu ni nani? Akiwanyoshea mikono wanafunzi wake, alisema: “Hawa ndio mama zangu na ndugu zangu! Mtu yeyote afanyaye mapenzi ya Baba aliye mbinguni, ndiye ndugu yangu, na dada yangu na mama yangu.”TVV 177.1

    Wote wanaompokea Yesu kwa imani huunganika naye kwa kiungo kinachozidi kile cha mwungano wa kijamaa cha kibinadamu. Waamini na watendaji wa mapenzi yake, yaani washikao neno lake, huwa na uhusiano zaidi kuliko mama wa kawaida wa hali ya kibinadamu. Ndugu zake wasingepata kitu zaidi kwake, isipokuwa wampokee Kristo kuwa Mwokozi wao.TVV 177.2

    Kutoamini kwao kutakuwa ni uchungu mkali sana unaowekwa kikombeni ukiandaliwa kwetu.TVV 177.3

    Uadui unaoandaliwa kwa wanadamu kwa ajili ya kupinga injili ulikuwa mchungu mkali katika maisha ya Yesu katika maisha ya kwao nyumbani. Ndugu zake walimtazamia kuwa mshauri wao. Waliona kuwa kama angalisema maneno yanayokubalika kwa Mafarisayo, angaliepukana na mabishano yasiyo ya lazima. Walifikiri kuwa alirukwa na akili kwa kujiweka katika haIi ya Uungu. Walijua kuwa Mafarisiyo walikuwa wakitafuta njia za kumshitaki, nao walidhani kuwa amewapatia njia za kutosha kumshitaki.TVV 177.4

    Hawakupima kazi aliyokuwa akifanya, wala hawakumhurumia katika matatizo yake. Mambo yake hayakujaliwa, wala yeye na maneno yake hayakujaliwa hata kidogo. Kwa hiyo alisikitishwa sana na hali yao; maana alieleweka vibaya, na kuumia vibaya sana.TVV 177.5

    Ndugu zake walithubutu kudhani kwamba wataweza kumfundisha ajue mambo ya kweli, Walimlaumu wazi katika mambo wasiyoyajua. Walidhani kuwa wanafanya mapenzi ya Mungu, kumbe hawakumwelewa hata.TVV 177.6

    Mambo haya yalifanya njia ya Yesu kuwa yenye miiba. Kwa hiyo maisha ya Yesu yalikuwa machungu huko kwao kwa watu wa kwao; na ilikuwa afadhali kwenda mahali pengine ambapo mambo hayo hayakuonekana. Alipenda kwenda kwao Lazaro, Maria na Martha, mahali ambapo palikuwa na utulivu na upendo alipata burudiko. Walakini alipata burudiko mara nyingi alipokuwa peke yake akiongea na Baba yake.TVV 177.7

    Watu walioitwa kufanya kazi kama ile ya Yesu ya matatizo, na kunenwa vibaya kwa ajili ya Kristo, katika nchi ya kwao wenyewe, watafarijika kwa kuwa Yesu naye alipambana na mambo ya jinsi hiyo. Anawaagiza wajiburudishe kwake na kwa Baba wa mbinguni.TVV 177.8

    Wanaompokea Kristo, hawawezi kuachwa kana kwamba ni yatima, wakabiliane na matatizo peke yao. Wao kama jamaa ya mbinguni, Yesu anawaagiza kumwita Baba yake kuwa Baba yao. Baba Mungu ana fadhili kubwa sana juu yao kuliko fadhili za baba wa dunia wanazoonyesha kwa watoto wao.TVV 178.1

    Wakati Mwebrania alipolazimika kujiuza kwa ajili ya umaskini, na kuwa mtumwa, jamaa wa karibu alipaswa kumkomboa. Tazama Mambo ya Walawi 25:25, 47-49; Ruth 2:20. Vivyo hivyo kazi ya kutukomboa humwangukia aliye wa jamaa yetu ya karibu. Kristo ndiye alikuwa jamaa yetu wa karibu. Amekuwa wa karibu zaidi kuliko baba, mama, ndugu, rafiki mpendwa yeyote. Bwana Yesu ni Mwokozi wetu. Sisi hatuwezi kufahamu upendo huo, lakini twaweza kujua kuwa ni wa kweli kwa njia ya maisha.TVV 178.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents