Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  15 — Yesu Ahudhuria Harusi

  Katika kijiji kidogo cha Galilaya walipokusanyika watu kwa karamu Ya arusi, Yesu alifanya mwujiza ili kuongeza furaha zaidi katika arusi. Hivyo ndivyo alivyoonyesha fadhali zake kwa watu, na jinsi alivyowahudumia. Katika jangwa yeye mwenyewe alikinywea kikombe cha masumbuko, sasa alikuja kuwanywesha watu kikombe cha baraka.TVV 74.1

  Kulikuwa na arusi huko Kana na Yusufu na Mariamu walihusika katika arusi hiyo, maana ni ya jamaa yao; na Yesu pia alihudhuria pamoja na wanafunzi wake.TVV 74.2

  Mariamu, mama yake, alikuwa amesikia habari za mafunuo yaliyotokea huko Yordani, wakati wa ubatizo wa Yesu. Habari hizi zilimfikirisha upya juu ya mambo aliyokuwa akiwaza kwa muda mrefu. Kazi ya Yohana Mbatizaji ilimchangamsha sana Mariamu. Alikuwa akiona hali ya Yesu, na kuamini kuwa ndiye Masihi, lakini alikuwa na mashaka pia. Alitamani siku ambayo atajidhihirisha wazi kuwa ndiye Masihi hasa.TVV 74.3

  Kifo kilikuwa kimewatenga Yusufu na Mariamu tayari; Yusufu alikuwa na mawazo sawa na Mariamu kabla ya kufa kwake. Sasa hakuna mtu ambaye Mariamu atamweleza mawazo yake ya matumaini, na mashaka pia. Aliyatafakari maneno ya Simioni, yaliyosema: “Nawe mwenyewe, upanga utaingia moyoni mwako.” Luka 2:35. Kwa hamu, alingoja Yesu arudi.TVV 74.4

  Kwenye arusi ya Kana alikutana na Yesu; mwenye upendo ule ule. Lakini alikuwa umebadilika. Uso wake ulikuwa hali ya mashindano aliyokuwa nayo jangwani. Na hali ya utukufu ilionyesha kuwa yeye anafanya mambo ya mbinguni. Alikuwa na kikundi cha watu waliokuwa wakimwita Bwana. Kikundi hiki kilimweleza Mariamu mambo waliyosikia na kuona kwenye ubatizo, na kwingineko. Watu walipokusanyika, ikawa hoihoi ya karamu. Na Mariamu alipoona kuwa macho ya watu yanamwangalia Yesu, alitaka sana ajionyeshe kuwa yeye ni mpendwa wa Mungu.TVV 74.5

  Ilikuwa desturi kuwa sikukuu ya ndoa huendelea siku kadha wa kadha. Katika mfulizo huo kabla sikukuu haijamalizika, divai iliwaishia. Mariamu alikuwa akihudumia kama jamaa, sasa alimwambia Yesu, “Hawana divai.” Maneno haya yalimaanisha kuwa Yesu atengeneze nyingine. Lakini Yesu alisema, mwanamke, nina nini nawe? Saa yangu haijaja bado”TVV 75.1

  Usemi huu sio wa kudharau, au kutokuwa na adabu. Katika desturi za watu wa mashariki, huo ndio usemi wa heshima na adabu. Kristo mwenyewe alitoa amri isemayo: “Mheshimu baba yako na mama yako.” Kutoka 20:12. Pote, katika arusi na katika msalaba, maneno ya mwisho ya Kristo kwa mama yake yalionyesha heshima na adabu na upendo.TVV 75.2

  Wakati wa ujana wake, alipokwenda hekaluni, Kristo alisema kwa.Mariamu: “Hamkujua ya kuwa inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” Luka 2:49. Sasa anarudia fundisho lile lile. Ilikuwa hatari kwa Mariamu kudhani kuwa uhusiano wake na Yesu, unampa haki ya kumfanya mwana wake, wala si Mwokozi wa ulimwengu. Kwa muda wa miaka thelathini alikuwa mwana wake akimtii, lakini sasa yapasa awe kwa kazi ya Baba, yaani kazi ya ukombozi. Kama Mwokozi wa ulimwengu, hapaswi kufungwa na uhusiano wa jamaa kiasi cha kumzuia asitimize kazi yake. Fundisho hili linatuhusu na sisi pia. Mvuto ya duniani, ushikamano wa jamaa, wala kitu kinginecho, visituvute tutoke katika mapito tuliyoagizwa na Mungu kupita.TVV 75.3

  Mariamu angepata wokovu kupitia kwa Kondoo wa Mungu peke yake. Uhusiano wake na Yesu haukuwa tofauti na uhusiano wa watu wengine na Yesu. Maneno ya Mwokozi yalipambanua wazi uhusiano wake na yeye, na uhusiano wake na Mungu. Uhusiano wa kuzaliwa tu hautaleta uhusiano upasao wokovu.TVV 75.4

  “Saa yangu bado haijaja.” Yesu alipotembea kati ya wanadamu, alikuwa akiongozwa hatua kwa hatua na mapenzi ya Baba. Kule kusema kwa Mariamu kuwa saa yangu haijaja bado, alisema maneno ambayo bado ni mawazo tu, ni mawazo yale aliyokuwa na matazamio ya kujidhihirisha wazi kuwa ni Masihi. Lakini saa haijaja bado. Sio kuwa mfalme, ila ni kama mtu mweye masikitiko na huzuni tu, ajuaye sikitiko.” Yesu alikubali kuchukua fadhaa za wanadamu.TVV 75.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents