Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Maonyo makali ya Yohana kwa wanafiki

  Yohana aliwakabili akiwa na maneno machungu haya: “Ninyi wazao wa nyoka, Nani aliyewaonya mwikimbie adhabu ijayo? Zaeni basi matunda yapasayo toba. Wayahudi wamejitenga mbali na Mungu, walikuwa wakiteseka na adhabu zake. Hii ndiyo ilisababisha watekwe na mataifa ya kishenzi. Kwa kuwa zamani Mungu aliwafanikisha, ndiyo sababu walidumu dhambini, huku wakidhani kuwa wangali Wapenzi wa Mungu. Walijivuna bure kwamba wao ni bora kuliko mataifa mengine; ndiyo sababu wanafanikiwa.TVV 51.1

  Yohana aliwaambia walimu wa Israeli kuwa kiburi chao, na uchoyo wao na ukatili wao, vimewafanya kuwa watu wa laana. Kufuatana na nuru yao, walikuwa bora kuliko wengine kama Mungu alivyowaagiza. Lakini sasa ni wabaya kuliko wengine. Mungu hawatumaini kutimiza kusudi lake tena. Mungu ataita wengine wafanye kazi yake.TVV 51.2

  Nabii alisema: “Sasa shoka limewekwa chini ya mti: kila mti usiozaa matunda mazuri, utakatwa na kutupwa motoni.” Ikiwa matunda ni mabaya, jina la mti haliwezi kuuokoa usiharibiwe. Yohana aliwaambia. Wayahudi kuwa, kama tabia zao hazipatani na amri za Mungu, wao sio wa Mungu kamwe.TVV 51.3

  Alisema, “Watakaohesabiwa kuwa raia wa ufalme wa Kristo, wataonyesha imani yao kama ushahidi. Wema, na haki vitaonekana katika maisha yao, Watawahudumia wahitaji, watawakaribisha wasiokuwa na makao, na wataonyesha mfano mwema wa utawa na unyofu.TVV 51.4

  “Mimi nawabatiza kwa maji, kwa ajili ya toba, lakini yeye ajaye nyuma yangu, ni mkuu, kuliko mimi, ambaye mimi sistahili hata kulegeza kamba za viatu vyake. Yeye atawabatiza katika Roho na kwa moto.” Isaya alikuwa amesema: “Bwana atawatakasa watu wake kwa Roho ya hukumu, na kwa Roho ya kuteketeza.” Isaya 4:4. Kwa wote watakaokubali uwezo wake, roho wa Mungu atateketeza dhambi. Waebrania 12:29. Lakini watu wakiambatana na dhambi, Roho wa Mungu ateketezaye dhambi, atawateketeza wao. Wakati wa kurudi mara ya pili kwa Kristo, waovu wote watateketezwa na kuangarnizwa; kwa pumzi ya kinywa chake na kwa mng’ao wa kufunuliwa kwake. 2 Wathesalonike 2:8. Utukufu wa Mungu ulelao uzima kwa watakatifu, utawateketeza waovu.TVV 51.5

  Siku za Yohana Mbatizaji, Kristo alikuwa karibu kutokea, ambaye ni sura ya Mungu, na tabia yake. Kuwako kwake kutadhihirisha dhambi za watu. Wasipokubali kuondolewa dhambi zao hawatakuwa washiriki wa ufalme wake. .TVV 52.1

  Hivyo ubatizo ulieleza ujumbe wa Mungu kwa Israeli. Watu wengi walitubu, wakaacha vyote ili wapate kutii. Watu wengi walimdhania kuwa ndiye Masihi. Lakini Yohana alipoona watu wengi wakimjia, alifanya kadiri awezavyo kuwaelekeza kwa yule ajaye.TVV 52.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents