Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  76 — Jinsi Yuda Alivyopoteza Roho Yake

  Historia ya Yuda huonyesha mwisho wa huzuni wa maisha ya mtu ambaye angeheshimiwa katika kazi ya Mungu. Kama yuda angalikufa kabla ya safari yao ya mwisho ya kwenda Yerusalemu angalihesabiwa kuwa mtu mashuhuri sana kati ya mitume kumi na wawili, ambaye angeacha pengo kubwa sana. Chuki ambayo imemfuata katika karne zote isingekuwako. Lakini tabia yake imedhihirishwa kwa ulimwengu kama onyo kwa wote wale watakaosaliti dhamana takatifu.TVV 403.1

  Tangu siku ile ya karamu nyumbani kwa Simon Yuda alikuwa amepata nafasi ya kukitafakari kitendo alichokuwa ameagana kukitekeleza, lakini kusudi lake lilikuwa halijabadilika. Kwa bei ya mtumwa akamuuza bwana wa utukufu.TVV 403.2

  Yuda kwa asili alikuwa na tabia ya kupenda fedha sana, lakini siku zote hakuwa mpotovu kiasi cha kutenda tendo baya kama hili. Aliilea roho ya uchoyo wa fedha mpaka ikapita upendo wake kwa Kristo. Kwa tendo moja ovu akajitolea mwenyewe kwa Shetani, kutumiwa katika kiwango cho chote kile kutenda dhambi.TVV 403.3

  Yuda alijiunga na wanafunzi wakati watu wengi walipokuwa wakimfuata Kristo. Alishuhudia matendo makuu ya Kristo ya kuponya watu, na kufukuza pepo wachafu, na kufufua wafu. Aliyatambua mafundisho ya Yesu kuwa bora zaidi ya yote yale aliyopata kusikia. alitamani kubadilishwa tabia na alitegemea kuwa hivyo kwa kujihusisha na Yesu. Mwokozi hamkukataa Yuda, alimpatia nafasi miongoni mwa wale kumi na wawili na alimjalia uwezo wa kuponya wagonjwa na kuwatoa pepo wachafu. Lakini Yuda hakujitoa moyo wake kwa Kristo kikamilifu. Hakuacha tamaa zake za ulimwengu wala kuzipenda fedha. Hakujiweka chini ya mvuto wa mbingu, bali alijitafutia tabia ya kukosoa na kushutumu.TVV 403.4

  Yuda alikuwa na mvuto mkubwa sana kwa wanafunzi wenzake. alijiona sana kutokana na sifa zake na aliwadharau ndugu zake kama walio duni. Alijisifu kuwa kanisa lisingestawi kama isingekuwa kwa sababu ya uwezo wake kama msimamizi. Machoni pake alijiona kuwa muhimu na kila mara alipenda mwonekano huo.TVV 403.5

  Kristo alimweka mahali ambapo angeona udhaifu wake na kujirekebisha, lakini Yuda alijiendeleza katika tamaa. Fedha chache alizokuwa akitunza kila mara zilikuwa zinamtia majaribuni. alipotenda kazi ndogo kwa ajili ya Kristo, alijilipa kutoka katika fedha hizo kidogo. Machoni pake hivi visababu vilitumiwa kama udhuru kwa vitendo vyake, lakini machoni pa Mungu alikuwa mwizi.TVV 404.1

  Yuda alichagua njia ambayo alitegemea Kristo aifuate katika kazi, alikuwa amepanga kuwa yohana Mbatizaji afunguliwe kutoka gerezani. Lakini Yohana aliachwa akatwe kichwa. Na Yesu, badala ya kulipa kisasi kwa ajili ya kifo cha Yohana aliondoka kwenda mahali pengine. Yuda alitaka hatua za ukakamavu zaidi zichukuliwe. Alifikiri kuwa kama Yesu asingaliwazuia wanafunzi kutekeleza mipango yao kazi ingefanikiwa zaidi. aliona kuwa madai ya viongozi wa kiyahudi hayakupata changamoto wakati walipodai Kristo atoe ishara kutoka mbinguni. Moyo wake ulikuwa wazi kufuata hisia za kutoamini na adui akaujaza uasi. Kwa nini Yesu alitabiri mateso na mashataka dhidi yake mwenyewe na kwa wanafunzi wake? Matumaini yake ya kupata cheo kikuu katika ufalme ujao yakatishwe tamaa?TVV 404.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents