Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kuthubutu kuingia katika Uwanja wa Shetani

    Kama Shetani akiweza kutushawishi ili tuwe mahali pa majaribu bila lazima, ajua kuwa atashinda bila shaka. Mungu atalinda watu wote wanaokwenda katika maagizo yake; lakini kutofanya hivyo ni kujiingiza katika kiwanja cha Shetat. Mwokozi ametuagiza akisema, “Kesheni na kuomba, msije mkaingia majaribuni ” Marko 14:38.TVV 63.2

    Kila mara tunapojiingiza mahali pa majaribu, huwa na wasiwasi, kwamba Roho wa Mungu ndiye anayetuogoza. Lakini Roho ndiye alimwongoza Yesu jangwani. Mungu akituingiza mahali pa majaribu, huwa na kusudi jema kwetu. Yesu hakwenda kulingana na ahadi za Mungu, kwenda mahali alipokatazwa pa, majaribu, wala hakukata tamaa, majaribu yalipomkabili. Hata sisi inatupasa kuwal hivyo. Soma 1 Wakorintho 10:13; Zaburi 50:14, 15.TVV 63.3

    Yesu alikuwa mshindi katika jaribu la pili, na sasa Shetani alijidhihirisha alivyo, ingawa alikuwa malaika aliyeanguka. Alikiri wazi kuwa yeye ndiye kiongozi wa maasi, na ndiye mungu wa ulimwengu huu. Akimpandisha Yesu juu ya mlima mrefu, alifanya falme zote za ulimwengu kupita mbele yake kama sinema. Akaona nuru ikimulika juu ya miji na majumba yake, akamwonyesha mashamba mazuri yenye rutuba, na miti yenye matunda. Hali ya laana na uovu ilifichika. Macho ya Yesu yaliona mambo hayo mazuri yenye kufanikiwa. Halafu sauti ya mjaribu ilisikika ikisema, “Haya yote nitakupa. . . . Kama wewe utanisujudia” Mbele ya Kristo kulikuwa na maisha ya huzuni, hali ngumu, na mapambano, na kifo cha aibu. Kristo angalijiokoa na hali hiyo mbaya kwa kukubali uku alioahidiwa na Shetani. Lakini kufanya hivyo kungalimletea kushindwa katika mapambano hayo. Je, Shetani atafaulu sasa? Ushindi utakuwa wa mwasi?TVV 63.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents