Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kristo asiyekuwa na dhambi, abatizwa

  Yesu hakubatizwa kwa kuungama makosa yake, kana kwamba anayo, bali alijifanya kama mwenye dhambi sawa na sisi, akichukua hatua zile zile tunazochukua sisi. Maisha yake ya taabu na uvumilivu wake, baada ya ubatizo, vilikuwa kielelezo kwetu.TVV 54.1

  Yesu alipotoka majini, alipiga magoti kuomba kando ya mto. Alikuwa sasa anaingia katika mapambano makubwa maishani mwake. Ingawa alikuwa Mkuu wa wakuu kuja kwake ni kama upanga uliochomolewa alani. Ufalme ambao atasimamisha, ni tofauti na ule Wayahudi wanaotamani. Ataonekana kana kwamba yeye ni mvunja sheria na mharibu wa mambo ya Israeli, ambaye atashutumiwa kama mwasi, na kutukanwa kama Belizebuli. Hakuna mtu aliyemwelewa, kwa hiyo itampasa aishi maisha ya upweke. Mamaye na nduguze hawakuelewa na kazi yake. Hata wanafunzi wake pia hawakuelewa.TVV 54.2

  Kama mmoja wetu, lazima achukue maovu yetu na matatizo yetu yote. Mtakatifu asiyekuwa na dhambi, lazima apate aibu ya dhambi. Mpenda amani lazima akae kwenye mashindano, mwenye ukweli lazima akae katika uongo na udanganyifu. Msafi, akae kwenye machukizo na uchafu, kila dhambi, kila ufedhuli, kila uchafu vyote viwe fungu lake, kana kwamba ni vyake hasa.TVV 54.3

  Lazima aitembelee na yeye mwenyewe. Kwake yeye aliyepokea hadhi ya kuwezesha ukombozi wa wanadamu, lazima autimize kikamilifu. Alijisikia kuwa na mzigo mzito mno, lakini alidumu kuwa imara.TVV 54.4

  Mwokozi alitoa moyo wake wote katika sala. Alijua jinsi dhambi ilivyokomaza mioyo ya watu, alijua jinsi ilivyo vigumu kwa watu kutambua kazi yake na kuikubali. Alimwomba Baba awalainishe wapate kuamini. Avunje pingu ambazo Shetani amewafunga, na apate kumshinda. Hakuna wakati ambao malaika walisikiliza sala yoyote kama hiyo. Baba mwenyewe ataijibu sala ya Mwanawe. Mbingu zilifunguka, nuru ya ajabu ikiwa mfano wa njiwa ikamshukia Yesu.TVV 54.5

  Waliokuwako hapo Yordani, ni wachache sana waliofahamu njozi hiyo, isipokuwa Yohana mbatizaji tu. Lakini hali ya kicho cha mbinguni iliwakalia wote waliokuwapo pale. Kristo aliyekuwa akielekeza uso mbinguni alitukuzwa kwa ajabu ambayo watu hawajaona, uso wa mtu uking’aa hivyo. Kutoka mbinguni, sauti ilisikika ikisema: “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye.”TVV 54.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents