Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wivu wa Herode Uliamishwa

  Ujumbe wa kigeni wa mamajusi uliwataharuki watu sana, walioishi Yerusalemu. Ujumbe huo ulipenya mpaka katika jumba la Mfalme Herode. Habari za uvumi zilizokuwapo, zilimfanya Herode ashuku mashambulio fulani. Kwa kuwa yeye alikuwa mwenye damu ya kigeni, alichukiwa sana na watu, ila usalama wake ulikuwa kwa Warumi tu. Lakini mtawala huyu mpya alikuwa na madaraka makuu, maana alikuwa amezaliwa katika ukoo wa mfalme. Herode alishuku kuwa makuhani wana njama pamoja na wageni kuchochea ghasia ili kumwondosha katika ufalme. Akiazimu kuupinga mpango huo kwa ujanja mwingi, aliwaita makuhani, akawauliza kuhusu mahali atakapozaliwa Masihi.TVV 29.5

  Ulizo hili lililotoka utawalani, ambalo limeulizwa na wageni, liliumiza kiburi cha walimu wa Kiyahudi. Uzembe wa kutojali unabii, ulimkasirisha mfalme. Alidhani kuwa wanajaribu kuficha ukweli, jinsi ulivyo. Kwa amri ya kifalme hawawezi kuthubutu kuzembea. Kwa hiyo aliwaamuru wachunguze na kujua mahali mfalme anayetazamiwa atakakozaliwa. Nao wakamwambia, “Katika Bethlehemu ya Yuda; maana imeandikwa na manabii: “Wewe Bethlehemu, nchi ya Yuda, ingawa u mdogo wewe, kati ya wakuu wa Yuda, Kwako atatoka mtawala, atakaye wachunga watu wangu Israeli.”TVV 29.6

  Sasa Herode aliwaita mamajusi kwa siri. Hofu na ghadhabu ilikuwa imemjaa. Lakini alijisimikiza, asionekane, akajifanya kana kwamba anamtukuza, Kristo aliyezaliwa. Aliwaagiza wageni wake, “Pelelezeni kwa bidii, mambo ya mtoto na mtakapomwona, niarifuni na mimi mahali mlipomwona, ili nami nikamsujudie.”TVV 30.1

  Makuhani hawakuwa gizani kama walivyojifanya. Habari iliyoletwa na malaika kwa wachungaji; ilikuwa imejulikana Yerusalemu, lakini Mafarisayo waliipuuzia. Ingaliwapasa wao kuwaongoza mamajusi katika safari yao, ili kuwapeleka kwa Yesu. Lakini badala ya wao kufanya hivyo mamajusi ndio walikuja kuwashtusha, kuhusu kuzaliwa kwa Masihi.TVV 30.2

  Kwa habari iliyoletwa na wachungaji na mamajusi ilikuwa sahihi, wangaliwakanusha makuhani wanaojidai kuwa ndio watoa habari za kweli ya Mungu. Walimu hawa walioelinmika wasingaliinamia wakafiri ili kuwasikiliza. Walisema kuwa, isingaliwezekana Mungu awapite, na kuzungumza na wachungaji wajinga, au na watu wasiotahiriwa. Wasingalishughulika kwenda hata Bethlehemu kuona kama habari hizo ni kweli. Hivyo wakawaongoza watu waone kuwa habari za kuzaliwa kwa Yesu ni hadithi tu za kuchekesha. Hapa ndipo ilikuwa mwanzo wa kumkana Yesu, kwa Mafarisayo na marabi. Ukaidi wao ulikuwa na kuwa chuki ya kumchukia Mwokozi.TVV 30.3

  Mamajusi waliondoka peke yao kutoka Yerusalemu. Kivuli cha usiku kikaingia. Lakini kwa furaha yao, waliona nyota tena, iliyowaongoza kwenda Bethlehemu. Waliondoka Yerusalemu wakiwa na matumaini zaidi kuliko walivyoingia, hali wakishangazwa na hali ya kutoamini kwa Wayahudi.TVV 30.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents