Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jinsi walivyopotosha Huduma ya Hema Takatifu

    Baada ya kurudi kutoka katika utumwa huko Babeli walijenga masinagogi katika nchi yote. Katika masinagogi hayo sheria ya Mungu ilifundishwa na Makuhani na waandishi. Shule za kufunza mambo ya haki zilifunguliwa. Lakini wakati wa utumwa huko Babeli watu wengi waliambukizwa desturi za kikafiri, nao waliingiza desturi hizi katika huduma za dini.TVV 15.3

    Kanuni za ibada na huduma zake zilikuwa zimeanzishwa na Kristo mwenyewe. Kanuni hizo zilikuwa zikimwonyesha Yeye na kufanya huduma kuwa maarufu. Lakini Wayahudi walipoteza maana yake ya kiroho, wakawa wakijiendeshea ibada tu isiyokuwa na maana yoyote, huku wakiamini kafara na kushika kanuni tu, kana kwamba watapata faida kwavyo. Badala ya kumwangalia yule anayeonyeshwa na vitu hivi, wao wakaamini vitu hivi tu. Wakajitungia kanuni zaidi ili kufanya mambo yawe bora. Kadiri shughuli hiyo ilivyokuwa, ndivyo upendo kwa Mungu ulivyopungua.TVV 15.4

    Watu waliotumainia mambo hayo zaidi, waliona kuwa hakuna utulivu mioyoni mwao. Na Shetani akawakatisha tamaa kabisa, hata wakawa na mawazo yaliyo kinyume cha Mungu, mpaka imani ya Waisraeli ikawa aibu tupu. Shetani alitaka kuwaaminisha watu kuwa matakwa ya Mungu hayawezekani kutii. Akasema kuwa, hata Waisraeli wameshindwa kuyashika, akatangaza kuwa, hata hawakushika sheria ya Mungu.TVV 15.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents