Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Haja ya uangalifu wa huruma

  Usimwaibishe mkosaji kwa ajili ya kutangaza makosa yake kwa watu wengine, wala usiliaibishe jina la Kristo kwa ajili ya kutangaza makosa ya mkristo waziwazi. Mkosaji lazima aonyeshwe makosa yake, ili ayaache. Lakini usihukumu au kulaumu. Katika kupo-nya mgonjwa wa moyo wa mtu kunahitaka kutumia uangalifu mwingi wa huruma. Upendo wa yule mtu wa Kalwari peke yake ndio unatosha kulishughulikia jambo hili. Kama ukifaulu katika jambo hili, “Utampo-nya mtu kutokana na mauti”, na “Utaufunika wingi wa dhambi.” Yakobo 5:20.TVV 251.2

  Lakini hata bidii hii inaweza kushindwa. Kisha Yesu alisema, “Chukua mtu mwingine au watu wawili mwende nao.” Kama hatawasikia wao pia, ndipo sasa shauri hili litaletwa mbele ya kundi lote la washiriki. Hebu washiriki wa kanisa wote waungane katika maombi wakirnsihi ndugu huyu apate kurudi. Roho Mtakatifu atazungumza naye kwa njia ya watumishi wake, wawasihi kwa ili ya Kristo, mpatanishwe na Mungu.” 2 Wakorintho 5:20. Mtu anayekataa maneno haya ya upatanisho huwa amejiondoa mwenyewe kutoka kwa Kristo, na hivyo hujifuta kutoka katika ushirika wa kanisa. Kwa hiyo Kristo alisema, ‘Na awe kwako kama mtu wa mataifa, na mtoza ushuru.” Lakini asidharauliwe na kutojaliwa na ndugu zake wa kwanza, mtendee kwa fadhili wala si kwa uhasama.TVV 251.3

  Mtu anayedharau njia zilizowekwa na Kristo, kwa ajili ya kuwarudisha wakosaji, husetiriki dhambi zile yeye mwenyewe. Soma Mambo ya Walawi 19:17. Dhambi ambazo tungezisahihisha, hutukalia sisi kama sisi ndio watendaji wake.TVV 251.4

  Haitupasi kuhesabu makosa kana kwamba ni maelezo ya mafafanuzi, kati yetu, kuyasema kwa wengine. Tunapotaka kurekebisha makosa ya ndugu zetu, inatupasa kuyafanya kisiri yasijulikane kwa watu hasa wale wasioamini. Jinsi tunavyo taka Kristo kutu-tendea ndivyo anavyotuamrisha kuwatendea wengine. “Mtakayoyafunga duniani, yatafungwa pia huko mbinguni, na mtakayoyafunga duniani, yatafunguliwa pia huko mbinguni.” Mathayo 16:19. Matokeo yenu ni ya milele.TVV 251.5

  Lakini haitupasi kubeba madaraka haya peke yetu. Maneno haya yakifuatwa kikamilifu Kristo hukubaliana nayo katika nikusanyiko wa kanisa, wanafunzi wakusanyikapo, kwamba ni wachache, au wengi, wakusanyikapo kwa jina la Yesu, atakuwa pamoja nao. Asema “Wawili wenu wakipatana katika jambo lolote duniani, wakiomba, litafanywa na Baba yangu aliye mbinguni.’Wakati Yesu akiwa katika mwili, alishiriki na wanafunzi wake, katika majanbu yao na kuwahurumia katika matatizo yao, na katika Uungu wake huwaunganisha katika kiti cha enzi cha Mungu.TVV 252.1

  Ahadi ya ajabu. Uwezo wote wambinguni hujiunga na ubinadamu ili kuvuta watu kwa Kristo.TVV 252.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents