Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kristo Aeleza Jinsi Petro Atakavyokufa

  Kabla ya kufa kwake, Yesu alimwambia Petro, “Niendako mimi huwezi kunifuata sasa, lakini utanifuata baadaye.” Kuhusu jambo hili alikuwa amejibu Petro Bwana, kwa nini mimi nisiweze kukufuata sasa? Mimi Nitautoa uhai wangu kwa ajili yako,” (Yohana 13:36, 37). Jaribu lilipokuja alishindwa lakini alikuwa apate nafasi nyingine ili athibitishe upendo wake kwa Kristo. Ili kwamba aimarishwe kwa ajili ya jaribu la mwisho la imani yake. Mwokozi alimfunulia maisha yake ya siku za usoni. Baada ya maisha yenye mafanikio, wakati ambapo uzee utamsogelea kwa hakika atamfuata Bwana wake. Yesu akasema; “wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyoosha mikono yako na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka.” Alisema neno hilo kwa hali ya kuonyesha ni mauti gani atakayomtukuza Mungu.”TVV 459.8

  Na hivyo Yesu alitabiri kunyosha mikono kwa Petro juu ya msalaba. Kisha akamwambia mwanafunzi wake, “Nifuate.” Petro hakuvunjwa moyo na ufunuo huo. Alijisikia kuwa radhi kupata mateso ya kifo cho chote kile kwa ajili ya Bwana wake. Hapo awali Petro alikuwa amempenda Kristo kama mwanadamu; sasa alimpenda kama Mungu. Sasa alikuwa tayari kushiriki pamoja na Bwana katika utume wake wa kafara. Na hatimaye alipoletwa msalabani kutokana na ombi lake mwenyewe alisulibishwa kichwa chini. Aliona kuwa ni heshima kuu mno kuteseka kama Bwana wake alivyoteseka. Kabla ya hapo Petro alijaribu kupanga kazi ya Mungu badala ya kungojea kufuata mpango wa Mungu. Lakini Yesu alimwambia “Nifuate.” Usinitangulie mbele. Acha mimi nitangulie mbele yako, na hutashindwa na adui. Petro alipokuwa akitembea kando kando ya Yesu alimwona Yohana akifuata nyuma yake. Naye akatamani kujua mambo yake ya mbele, na akamwambia Yesu, “Bwana, na huyu je? Yesu akamwambia, Ikiwa nataka huyu akae hata nijapo, imekupasa wewe? Wewe unifuate mimi.TVV 460.1

  Petro alipaswa kutambua kuwa Bwana wake atamfunulia yale yote aliyopasa kuyafahamu. Kule kusema juu ya Yohana kuwa “Ikiwa nataka huyu akae hata nijapo” Yesu hakutoa uthibitisho wo wote kuwa mwanafunzi huyu ataishi mpaka kurudi mara ya pili kwa Bwana na hata kama ni mapenzi yake kuwa iwe hivyo, haingehusiana kwa vyo vyote vile na kazi ya Petro. Utii ulikuwa ndiyo wajibu wa kila mmoja.TVV 460.2

  Ni watu wangapi siku hizi wanapenda kufahamu mambo ya watu wengine, wakiwa na shauku kutaka kujua majukumu yao, huku wakiwa katika hatari ya kupuuza wajibu wao! Ni jukumu letu kumtazama Kristo na kumfuata. Kwa kumwangalia yeye, tutabadilishwa.TVV 460.3

  Yohana aliishi mpaka kushuhudia kuharibiwa kwa Yerusalemu na hekalu lake, ambao ni mfano wa uharibifu wa mwisho wa ulimwengu. Alimfuata Bwana wake mpaka siku zake za mwisho. Petro alikuwa amerejeshwa katika utumishi wa utume wake lakini heshima aliyokuwa amepokea kutoka kwa Kristo haikumpa ukuu wo wote dhidi ya ndugu zake. Kristo alikuwa ameliweka hili wazi katika kujibu swali la Petro, “Bwana, na huyu je?” Alimwambia, “Imekupasaje wewe? Wewe unifuate mimi.” Petro hakutukuka kama kiongozi wa kanisa. Alikuwa na mvuto mkubwa katika kanisa, lakini somo Kristo alilomfundisha kando ya bahari ya Galilaya, Petro alilizingatia katika maisha yake yote.TVV 461.1

  Akiyaandikia makanisa, Petro alisema; “Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo . . . lichungeni kundi la Mungu ... si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi. Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka.” Petro 5:1-4.TVV 461.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents