Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Shetani atenda kazi kwa kujificha

  Ndivyo itakavyokuwa katika wakati wa mapambano ya mwisho, baina ya haki na uovu. Wakati wanafunzi wa Yesu watakapopata nguvu mpya na maisha mapya, Shetani naye atawavuvia wafuasi wake nguvu mpya na juhudi mpya. Kwa hila na ujanja wa muda mrefu alivyopata katika mapambano haya, Shetani atajigeuza hali katika mapigano haya, aonekane kana kwamba ni malaika wa nuru. Watu wengi hutega masikio kusikiliza mafundisho ya Shetani, na roho zenye kudanganya. 1 Timotheo 4:1.TVV 138.4

  Viongozi na walimu wa Israeli walidharau njia ambazo wangetumia ili washinde roho zidanganyazo za kishetani. Njia hizo ni kulifuata Neno la Mungu, ambalo lilimshindisha Kristo huko jangwani. Kwa kulitafsiri vibaya neno hilo, likaeleweka kinyume cha maongozi ya Mungu. Wakati ufafanuzi wa kinyume cha ukweli ulivyo hasa. Kwa hiyo neno la Mungu likapotoshwa, lisiwe na uwezo wake, na badala yake udanganyifu wa Shetani ukakubaliwa kana kwamba ndiyo ukweli.TVV 139.1

  Historia inajirudia. wakati wetu huu, waongozi wa dini huharibu imani yao na hali wanalo neno la Mungu mikononi mwao. Hukatakata vipande na kutia mawazo yao, badala ya neno la Mungu. Hii ndiyo sababu ushenzi umezidi na maovu yamejaa popote.TVV 139.2

  Wale wanaoacha kufuata maandiko matakatifu yaliyo dhahiri, ambayo ni uwezo wa Mungu, hukaribisha roho za mashetani. Tuhuma na kupapasapapasa maandiko wazi ya neno la Mungu, hufungua mlango wa kuingiza ibada ya roho chafu, hata kwa wale wanaojiita kuwa ni wakristo. Wajumbe wa Shetani huenda bega kwa bega na mahubiri ya injili. Watu wengi hujitia kuchunguza roho hizi za mashetani, na wakiisha kuona kuwa kuna nguvu isiyo ya kibinadamu, huendelea kudumu hapo mpaka hata wao wakapata hali hiyo pia. Mwisho uwezo wa mtu hushindwa, na mtu hutekwa nyara bila habari, huwa kama mwenye pepo wa Kapernaumu. Walakini hali yake si kama ya yule.TVV 139.3

  Anaweza kushinda kwa nguvu za Neno la Mungu. Tunapotamani kujua neno la Mungu na kulifuata, na kufanya mapenzi yake, ahadi yake kwetu ni “Mtaifahamu kweli, na kweli itawaweka huru.” “Kama tu atataka kufanya mapenzi ya Mungu, atajua kama mafundisho haya ni ya Mungu.” Yohana 8:32; 7:17. Kwa njia ya kuziamini ahadi hizi, kila mtu aweza kuokolewa na mitego hii na makosa yenye kushikilia mtu dhambini.TVV 139.4

  Saa kwa saa walifurika kuja na kwenda, maana hakuna ajuaye kuwa Mponyaji atakuwa bado yuko hapo. Kapernaumu ilikuwa haijaona siku yenye shughuli kama hii. Anga ilijazwa na sauti za shangwe na shukrani kwa ajili ya kuponywa. Mwokozi alifurahia uwezo wake wa kuwaponya wenye dhiki.TVV 139.5

  Watu walipoondoka, usiku ulikuwa umeendelea sana, na ukimya wa usiku uliobaki ukawa wa kupumzika, nyumbani kwa Simoni. Mchana wa hoihoi ulikuwa umepita, na wakati wa kimya cha usiku kiliendelea. Lakini katikati ya kimya hicho, watu wakiwa wamelala .... Mwokozi alitoka akaenda mahali pa kimya kuomba.TVV 139.6

  Kila mara Yesu aliwaruhusu wanafunzi wake, ili akawasalimu katika miji yao, na kupumzika. Lakini ilikuwa vigumu kuacha kazi kwa ajili ya makutano ya watu. Mchana kutwa alishughulika na jioni, au asubuhi mapema alikwenda mlimani kuongea na Baba yake. Mara nyingi aliomba usiku kucha, ndipo akaja kufanya kazi yake kwa watu.TVV 140.1

  Asubuhi mapema Petro na wenzake walikula kwa Yesu wakisema kuwa watu wanamtafuta. Wakuu wa Yerusalemu wanamtafuta kumwua, hata watu wa kwao pia wanataka kumwua, lakini huko Kapernaumu alikaribishwa kwa furaha. Ndipo matumaini ya wanafunzi yakapata nguvu, maana walikuwa na wasiwasi. Ilikuwa, kwamba wapenda uhuru katika Kapemaumu ndio walikuwa watetezi wa ufalme mpya. Kwa mshangao walisikia maneno ya Kristo yakisema: “Twende tu katika miji mingine, ili nipate kuhubiri huko pia. Maana nilikuja kwa ajili hiyo.” Marko 1:38.TVV 140.2

  Yesu hakuridhika kusifiwa kama mtenda miujiza. Watu walipokuwa na matumaini kuwa amekuja kama mfalme ili kuusimamisha ufalme duniani, alitaka kugeuza mawazo yao kuyaelekeza mbinguni, yaani mambo ya kiroho.TVV 140.3

  Mashangilio ya watu hawa wapuuzi yalimchukiza sana. Heshima na sifa wanazopewa watu wa dunia, kwa Kristo zilikuwa ngeni tu. Yesu hakutumia njia za watu ili kujulikana. Yesu hakupiga kelele, wala kujionyesha kwa njia yoyote. Alitoa haki kwa uaminifu tu. Isaya 42:2, 3.TVV 140.4

  Katika maisha ya Yesu hakikuwako kitu cha kujionyesha wala hali ya kutaka pato. Kristo alijificha ndani ya Mungu; na Mungu alijidhihirisha katika Mwana wake. Jua la Haki halikung’aa ulimwenguni kwa fahari ili kufanya nuru kwa utukufu wake, jua la Haki hilo lilitokea kimya, polepole, likang’aa gizani, likaleta uhai duniani. Ndivyo jua la haki hung’aa kwa mabawa ya kuponya. Malaki 4:2.TVV 140.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents