Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  25 — Mwito Kando ya Bahari

  Siku ilikuwa inakucha huko katika bahari ya Galilaya Wanafunzi walikuwa wamechoka kwa kazi ya usiku isiyokuwa na matokeo yoyote yaliyo mazuri, nao walikuwa wangali katika mashua zao katika ziwa la Galilaya. Yesu alikuwa amekuja kupunga hewa baharini asubuhi. Alitaka ajipumzishe kidogo kutokana na makutano yaliyokuwa yakimfuata siku kwa siku. Lakini watu walianza kukutanika, na mara akawa amezungukwa pande zote.TVV 131.1

  Kwa kuepuka msongamano wa watu, Yesu aliingia ndani ya mashua ya Petro, akamwambia aisogeze baharini kidogo. Mahali hapo aliweza kuonekana na kusikika vizuri na watu wote. Kutoka baharini hapo ndani ya mtumbwi, aliwafundisha watu waliokuwa wakisimama pwani. Aliyetukuzwa na mbingu alikuwa akiutangaza ufalme wake katika hewa, mbele ya watu. Ziwa, milima, uwanda mweupe, mwangaza wa jua, vyote hivyo vilikuwa vielelezo vya mafundisho yake, navyo viliwaingia watu kabisa. Hakuna fundisho lililopotea bure. Kila ujumbe ulipokelewa na watu kama neno la uzima wa milele.TVV 131.2

  Mambo kama haya ndiyo nabii alisema: “Nchi ya Zabloni na nchi ya Naftali, kuelekea bahari, ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa, Watu waliokaa gizani wameona mwanga mkuu na waliokaa katika uvuli wa mauti, Nuru kuu imewazukia.”TVV 131.3

  Yesu akiangalia vizazi, aliwaona watu wake waaminifu wakiwa gerezani na katika majumba ya hukumu, na katika majaribu, na dhiki na mateso. Maneno yaliyonenwa kwa watu waliokusanyika pwani ya ziwa la Genesareti, yalikuwa yakizungumzwa pia kwa watu wote watakaokuwa katika giza, majaribu, dhiki na mateso. Maneno yaliyonenwa ndani ya mtumbwi yataendelea kusikika kwa watu, yakiwapa tumaini mpaka mwisho wa dunia.TVV 131.4

  Mahubiri yalipomalizika, Yesu alimwambia Petro asogeze mtumbwi majini zaidi, apate kuvua. Lakini Petro alikata tamaa. Usiku kucha alikuwa akivua, asipate chochote. Wakati wa saa za upweke, alikuwa akifikiri habari za Yohana Mbatizaji, akiteseka gerezani, na habari za matazamio ya Yesu ya baadaye, habari za wafuasi wake, habari za kufaulu mgeuza Yuda, na habari za ukorofi wa makuhani na marabi. Alipoona kuwa hakupata kitu chochote katika nyavu zake, alikata tamaa kabisa. Akasema: “Bwana, tumesumbuka usiku wote, mpaka kumekucha; wala hatukupata kitu, walakini kwa ajili ya neno lako, nitatupa nyavu majini.”TVV 132.1

  Baada ya kusumbuka usiku kucha bila kupata kitu, ilionekana kuwa ni kazi bure kutupa nyavu baharini. Lakini kwa kuwa walimpenda Bwana wao, walitii. Simoni na ndugu yake walitupa nyavu majini. Walipojaribu kuzivuta, zilikuwa zimejaa samaki tele, mpaka akamwomba Yakobo na Yohana kusaidia. Waliposhusha samaki mitumbwi yote ilikuwa imejaa kabisa karibu kuzama.TVV 132.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents