Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Alipokewa Kwa Magari ya Malaika

  Wanafunzi walipokuwa wangali wakikaza macho mbinguni, malaika wawili wenye sura ya wanadamu, wakasema: “Enyi watu Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.”TVV 469.2

  Malaika hawa ambao ni wenye hadhi kuu katika malaika wote, walikuwa ni wale waliokuja kaburini kwa Yesu wakati wa kufufuka kwake. Walitamani kuungana na kundi la malaika waliokuja kumlaki Yesu, lakini katika kuwahurumia wale walioachwa na Yesu walibakia kuwafariji.TVV 469.3

  Kristo alikuwa amepaa juu katika mwili wa binadamu Yesu yule yule aliyekula pamoja nao, na aliyekuwa siku ile amepanda mlima wa Mizeituni pamoja nao. Malaika waliwahakikishia kuwa, ni Yule Yule waliyemwona akienda zake mbinguni, ndiye atakayekuja tena jinsi iyo hiyo alivyokwenda mbinguni. Atakuja “na mawingu; na kila jicho litamwona.” “Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.” “Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote, pamoja naye ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake.” Ufunuo 1:7; 1 Wathesalonike 4:16; Mathayo 25:31.TVV 469.4

  Hivyo ndivyo itakavyotimizwa ahadi yake Bwana kwa wanafunzi wake; “Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi nanyi mwepo.” Yohana 14:3.TVV 470.1

  Baada ya mateso na kusulibishwa kwa Kristo maadui wa wanafunzi walitumaini kuwaona wakionyesha huzuni na kukata tamaa. Lakini badala ya hayo waliwaona wakichangamka na kufurahi kwa ushindi na nyuso zao ziking’aa kwa furaha isiyokuwa ya duniani. Kwa shangwe walisimulia hadithi ya ajabu ya kufufuka na kupaa kwa Kristo, na ushuhuda wao ulipokelewa na wengi.TVV 470.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents