Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  11 — Ubatizo wa Yesu

  Ujumbe wa nabii wa jangwani ulifika mpaka milimani, wakaapo wakulima, na mpaka baharini kwenye wavuvi. Watu hawa wanyenyekevu waliamini. Katika Nazareti ilisemwa kwamba, Yusufu, Seremala na mmoja ambaye ndiye Yesu walimwamini ujumbe. Wakati wa Yesu umekuja. Alimwaga mamaye, akajiunga na wengine kwenda huko Yordani kwa nabii.TVV 53.1

  Yesu na Yohana mbatizaji walikuwa binamu, yaani ndugu kwa baba au kwa mama walakini walikuwa hawajaonana. Na sasa mambo yamewakutanisha. Muda ulikuwa haupo wa kukabiliana kama huu.TVV 53.2

  Yohana alikuwa na habari za kuzaliwa kwa Kristo, na hali yake ya maisha safi bila dhambi. Alimwamini kuwa ndiye Masihi. Lakini kwa kuwa Yesu hakujidhihirisha wazi, bali alikuwa katika hali ya ukimya, jambo hili lilitia wasiwasi na mashaka kumhusu. Walakini ubatizo ulingojea wenye imani. Ilijulishwa kwa Yohana kuwa Masihi atakuja kwake ili ambatize, na itakuwa ndiyo mwanzo wa kazi yake.TVV 53.3

  Yesu alipokuja kwa Yohana ili abatizwe, Yohana aliona utawa kwake, ambao hajawahi kuona hali kama hiyo kwa mtu yeyote. Kuwako kwake kulikuwa kwa hali ya kicho cha ajabu. jambo hili lilipatana jinsi alivyofunuliwa kabla, kumhusu Masihi. Sasa, inakuwaje yeye awe mwenye dhambi, hata ahitaji ubatizo? Inakuwaje kwake asiye dhambi ahitaji ubatizo wa kuoshwa dhambi?TVV 53.4

  Wakati Yesu alipotaka kubatizwa, Yohana alisema: Mimi ndiye ninahitaji kubatizwa na wewe, na wewe waja kwangu? Lakini Yesu alimjibu, Acha mambo hayo, maana hivyo ndivyo itakuwa kutimiza sheria. Basi akaacha. Kisha Yesu alipobatizwa, alitoka majini mara moja, na tazama, mbingu zilifunguliwa, akashuka Roho wa Mungu, kama njiwa, akamkalia.TVV 53.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents