Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  6 — Tumeiona Nyota Yake

  “Sasa, wakati Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi, siku za mfalme Herode, mara wakaja Mamajusi (watu wenye hekima) kutoka mashariki huko Yerusalemu wakisema, “Yuko wapi aliyezaliwa, Mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tumeiona nyota yake upande wa Mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.”TVV 28.1

  Mamajusi hawa wa mashariki wamo katika kundi la watu wenye mali, na wenye hekima na wataalam. Baadhi yao walikuwamo watu watawa, waliojifunza na kuchunguza mambo ya asili. Nao waliheshimiwa kwa ajili ya utawa wao na hekima yao. Katika watu wa tabia hii ndimo mamajusi hao walitoka waliokuja kwa Yesu.TVV 28.2

  Mamajusi hawa walipochunguza nyota za mbinguni waliona utukufu wa Mungu, ambaye ni Muumbaji. Walipojifunza juu ya elimu hiyo, na walipata ujuzi kamili, waligeukia maandiko ya Waebrania ili wayaelewe. Katika nchi yao kulikuwako na manabii waliotabiri juu ya kuja mwalimu wa asili ya Mungu. Utabiri wa Balaam ulikuwa ukipokelewa na vizazi kwa muda wa kane nyingi. Lakini katika Agano la kale, mamajusi walijifunza kuwa kuja kwa Mwokozi kulikaribia. Ulimwengu wote utajazwa na utukufu wa Bwana.TVV 28.3

  Mamajusi walikuwa wameona nuru ya ajabu huko mbinguni, wakati Utukufu wa Mungu ulipoangaza katika vilima vya Bethlehemu. Nyota yenye kung’aa ilionekana na kuangaza kwa muda. Jambo hilo lilivutia watu na kuwafikirisha. Nyota hiyo ilikuwa ni kundi la malaika wengi wenye kung’aa, lakini mamajusi hawakujua jambo hili. Lakini waliona kuwa ilikuwa nyota yenye jambo maalum kwa ajili yao.TVV 28.4

  Nyota hiyo isingekuwa ni mjumbe kuhusu Masihi aliyeahidiwa? Soma Hesabu 24:17. Mamajusi walipokea nuru ya mbinguni iliyotumwa kama mjumbe wa kweli sasa iling’aa kwao zaidi. Kwa njia ya ndoto waliagizwa waende kumtafuta Mkuu aliyezaliwa.TVV 28.5

  Nchi ya mashariki ilijaa na vitu tele vya thamani, kwa hiyo mamajusi hawakuondoka kwenda na mikono mitupu. Utajiri mkubwa kabisa ulitwaliwa kuwa sadaka ya kwenda nayo. Walimpelekea yeye yule ambaye watu wote hubarikiwa naye.TVV 29.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents