Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Nafasi ya Mwisho ya Pilato

    Hata wakati huo Pilato hakuachwa atende mambo kigizagiza. Mke wake alipewa ndoto na malaika akaona kuwa anaongea na Mwokozi. Mke wa Pilato hakuwa Myahudi, lakini alipomwona Yesu katika ndoto, alimtambua kwamba ni Mwana wa Mungu. Alimwona Pilato akimpiga Yesu mijeledi, baada ya kutamka kuwa: “Sioni hatia kwake.” Alimwona akimtia Kristo mikononi mwa wauaji. aliuona msalaba umesimami-shwa na dunia ikiwa imetandwa na giza nene, na alisikia kile kilio cha fumbo; “Imekwisha.”TVV 414.1

    Tena aliona tukio jingine. Alimwona Kristo ameketi katika kiti cha enzi katika wingu cheupe na wale waliomuua wakikimbia mbele ya utukufu wake. Kwa kilio cha kutisha alisituka na mara moja alimwandikia Pilato, maneno yenye onyo. Mtumishi alipenya katikati ya watu kumpatia barua kutoka kwa mkewe, ambayo ilisema: “Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake.”TVV 414.2

    Uso wa Pilato ulibadilika, alichanganyikiwa na michomo moyoni iliyohitilafiana. Wakati alipokuwa akisitasita katika kuamua, makuhani walikuwa wakichochea mawazo ya watu. Sasa alifikiria desturi ingetumika kumwachilia Kristo. Ilikuwa desturi yao wakati wa sikukuu hii kumfungulia mfungwa mmoja aliyependekezwa na watu. Hakukuwa na sheria yo yote katika desturi hii, lakini ilithaminiwa mno na Wayahudi. Katika muda huo Warumi walikuwa na mfungwa mmoja aitwaye Baraba, aliyekuwa akingojea kunyongwa. Mtu huyu alikuwa na kusudi la kupindua serikali. Alikuwa mwizi na mnyang’anyi aliyejipatia mali kwa nguvu. Alikuwa amechochea watu dhidi ya Serikali ya Warumi na kupata wafuasi. Alikuwa akidai kuwa anaendesha mambo ya dini; lakini alikuwa jambazi sugu aliyefanya vitendo vya uasi na ukatili.TVV 414.3

    Pilato alidhani kuwa kama akiwapa watu uchaguzi kati ya huyo na Mwokozi, ataamsha hisia ya kutenda haki mioyoni mwao. “Mnataka niwafungulie yupi? yule Baraba, au Yesu aitwaye Kristo?” Watu walijibu kama ngurumo ya wanyama wa porini wakisema: Tufungulie “Baraba!” Akidhani kuwa watu hawakuelewa vizuri swali lake, Pilato aliuliza: “Je! mnataka niwafungulie Mfalme wa Wayahudi?” Watu wakapiga kelele wakisema: “Mwondoe huyu, utufungulie Baraba!” “nimtendeeje yesu aitwaye Kristo?” Mashetani, wakiwa katika mfano wa wanadamu na kuchangamana na watu walijibu kile kilichotazamiwa: “Asulubishwe.”TVV 414.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents