Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kanuni zisizokuwa na maana

    Wayahudi walipotosha sheria kabisa, hata ikageuka kuwa mzigo mzito kwa watu, na wakafanya kuishika kuwe jambo lisilovumiliwa. Myahudi hakuruhusiwa kuwasha moto, au kuwasha mshumaa siku ya Sabato. Hivyo watu waliwategemea watu wa mataifa kuwafanyia mambo yale waliyokatazwa kufanya wao wenyewe. Walidhani kuwa wokovu ulikusudiwa kwa Wayahudi tu, na kanuni za watu wengine zilikuwa ovyo tu. Lakini Mungu hakutoa sheria ambayo haiwezi kutiiwa na watu wote.TVV 109.2

    Katika hekalu, Yesu alikutana na mtu aliyekuwa ameponywa. Alikuja kutoa sadaka ya dhambi, na sadaka ya shukrani kwa rehema alizopata. Yesu aliwajulisha kwake. Mtu yule alishangilia kwa kukutana na Mponyaji wake. Bila kujali uhasama wanaomfanyia Yesu, aliwaeleza Mafarisayo kuwa huyu ndiye aliyeniponya. Kwa hiyo walimsumbua Yesu, wakakusudia kumwua, kwa sababu anavunja Sabato.TVV 109.3

    Yesu alifikishwa katika bunge la Sanhedrin ili kujibu mashtaka hayo. Kama Wayahudi wangekuwa wanajitawala, mashitaka hayo ya kuvunja Sabato yangalileta kifo kwa Yesu. Lakini mashitaka ya jinsi hiyo hayana uzito wowote katika mahakama ya Kirumi. Mambo mengine walitumaini kuwa yatawasaidia. Kristo alikuwa na mvuto mkubwa kwa watu, kuliko Mafarisayo. Makundi ya watu hayakupenda hotuba za Marabi kama zile za Yesu. Alikuwa akinena maneno ya kweli ya Mungu, wala si kama mlaumuji na msutaji mwenye kuhukumu. Kwa njia ya mafundisho yake na matendo yake ya huruma alivunja nguvu za kanuni za wanadamu, alitoa neno dhahiri, na kuudhihirisha upendo wa Mungu.TVV 109.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents