Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Petro Ashindwa

    Lakini mwanamke aliyekuwa bawabu mlangoni, alimwangalia sana Petro, akamwona kuwa mwenye masikitiko na wasiwasi, akamhisi kuwa ni mmoja katika wanafunzi wa Yesu. Akitaka kujua akamwuliza: “Wewe nawe u mmoja wao?” Petro alishituka na kuchanganyikiwa: akijifanya kana kwamba hana habari juu ya mambo hayo. Lakini mwanamke aliendelea kukuzania hivyo. Petro akalazimika kujibu na kusema kwa hasira: “Sijui usemalo.” Hili lilikuwa kanusho la kwanza, na mara ile jogoo akawika. Katika hali ya kutojali, Petro alikuwa amejiweka katika hali ya kuwa mwepesi kwa majaribu.TVV 399.2

    Watu walimkazia macho mara ya pili. Na akasutwa kuwa ni mmojawapo wa wanafunzi wa Yesu. Sasa Petro akaapa, na kusema: “Mimi simjui mtu huyu.” Saa moja ilipita, wakati jamaa ya mtu yule aliyekatwa sikio na Petro huko katika bustani aliposema: “Je! mimi si nimekuona wewe bustanini pamoja naye?” “Hakika na huyu alikuwa pamoja naye, kwa kuwa yeye pia ni Mgalilaya.” Kusikia hivyo Petro alijaa hasira. Ili kuwadanganya hasa waliokuwa wanamhoji na kuthibitisha msimano wake, Petro sasa akamkana Bwana wake kwa kuapa na kulaani. Kwa mara nyingine jogoo aliwika. Petro aliposikia jogoo akiwika, aliyakumbuka maneno aliyoambiwa na Yesu, “Kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu.” Marko 14:30.TVV 399.3

    Wakati kiapo cha aibu kilipokuwa kingali kipya mdomoni mwa Petro na mlio wa jogoo ungali ukisikika masikioni, Mwokozi aligeuza uso wake akamtazama usoni masikini mwanafunzi wake. Kwa wakati huo macho ya Petro yakavutwa kumwangalia Bwana wake. Katika ule uso mpole aliona huruma na huzuni na sio hasira.TVV 400.1

    Kuutazama ule uso wa huzuni, ile midomo iliyotetemeka, moyo wake ulichomwa kama na mshale. Petro alikumbuka ahadi aliyoahidi, muda kitambo uliopita, wakati Mwokozi alipomwambia kuwa, atamkana mara tatu usiku ule. Petro sasa akatambua jinsi Bwana alivyokuwa amesoma sawasawa mawazo yake yenye udanganyifu ambao haukujulikana kwake yeye. Wimbi la kumbukumbu likafunika. Uvumilivu wa Mwokozi, kusitahimili kwake yote hayo yalikumbukwa. Akakumbuka kwa hofu juu ya uongo wake na ushuhuda wake katika kumkana Bwana kwa kuapa. Mara akaona mkono wa mtu mkorofi ukiinuliwa kumpiga Bwana wake usoni. Akiwa hawezi kuvumilia, zaidi hali hiyo, aliharakisha kutoka katika ukumbi huo akiwa amevunjika moyo. Aliendelea katika upweke na giza akiwa hajui wala kujali aendako. Mwisho akajikuta amefika katika Gethsemani.TVV 400.2

    Alikumbuka kwa uchungu mwingi jinsi alivyokuwa na maumivu makali akiomba peke yake, pia alikumbuka agizo Yesu alilowaagiza akisema: “Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni.” Mathayo 26:41. Jambo hili lilikuwa mateso rohoni mwake akijua kuwa amemwongezea Mwokozi mzigo wa udhilifu na huzuni. Petro akaanguka chini kifudifudi akitamani kufa. Kama saa zile walipokuwa katika bustani wanazitumia katika kukesha na kuomba, Petro asingelikuwa katika hali ya kutegemea nafsi yake dhaifu. Wala asingalimkana Bwana wake. Kama wanafunzi wangalikesha pamoja na Yesu katika mateso yake wa-ngalikuwa tayari kuyaona pia mateso yake msalabani. Katikati ya saa ngumu ya huzuni, tumaini lingewasha giza lao na kuitegemeza imani yao.TVV 400.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents