Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mioyo Yao Ilivutiwa Kwa Mgeni Huyu

  Walipokuwa wakisafiri jua lilikuwa limekuchwa na wafanya kazi mashambani walikwisha rejea kutoka makazini mwao. Wanafunzi walipokaribia kwao, mgeni wao alifanya kana kwamba ana haja kuendelea mbele Lakini wanafunzi wale walitamani kusikia maneno zaidi kutoka kwake. Ndipo wakamshawishi wakisema: “Kaa pamoja nasi.” Lakini alielekea kukataa, nao wakamshurutisha, “Kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha.” Yesu akakubali, “Akaingia ndani kukaa nao.” Kama wanafunzi wasingelimshurutisha kukaa nao, wasingalifahamu kuwa aliyefuatana nao alikuwa Bwana Aliyefufuka. Kristo hajilazimishi kuwa pamoja na mtu ye yote. Ataingia kwa furaha katika nyumba yo yote, lakini ikiwa watu hawajali kumsihii akae, atapitiliza.TVV 451.2

  Chakula cha kawaida cha jioni kiliandaliwa na kuwekwa mbele ya mgeni aliyekuwa ameketi mahali pa heshima. Sasa aliweka mikono yake juu, akakibariki chakula, kama vile Bwana wao alivyokuwa akifanya. Wanafunzi wakashangaa sana. Walitazama tena kuona mikono iliyopigiliwa kwa misumari. Wakaona Lo, kumbe ni Bwana Yesu! Waliondoka kumwangukia miguuni, lakini akatoweka mbele yao. Wakapatazama mahali alipokuwa ameketi yule ambaye hivi karibuni mwili wake ulikuwa umelala kaburini, nao wakaambiana, “Je! mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani na kutufunulia Maandiko?”TVV 451.3

  Wakiwa na habari hizi moto moto za kutawanya, uchovu wao na njaa vilitoweka. Walikiacha chakula bila kukionja wakaharakisha kupitia njia ile ile waliyoijia, kwenda kuwapasha habari wanafunzi wenzao mjini. Walipandisha miinuko, wakiteleza juu ya miamba, wakitamani kwenda haraka kuliko walivyoweza. Wakapotea njiani, lakini wakaipata njia tena. Wakati mwingine wakikimbia, na kuteleza, waliendelea na safari, huku mwenzao asiyeonekana akiwa kando kando yao njiani kote.TVV 451.4

  Usiku ulikuwa wa giza nene, lakini Jua la Haki liliku wa likiwamulikia. Walijiona kana kwamba wamo katika ulimwengu mpya. Kristo amefufuka walirudia rudia kusema hivyo. Ni lazima wawambie wale wenye huzuni kisa cha ajabu kilichotukia njiani kwenda Emau. Ni lazima waeleze juu ya yule Aliyejiunga nao njiani. Walibeba ujumbe mkuu uliowahi kutolewa habari njema ambazo kwazo tumaini la jamii ya wanadamu lilitegemea tangu sasa na milele.TVV 452.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents