Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Nia ya ubinafsi yadhihirishwa

    Ndugu hawa wa Yesu walisema hayo kutokana na nia yao ya ubinafsi na kutaka makuu. Kisha Yesu aliwaambia: “Saa yangu haijafika bado, lakini saa zenu siku zote zipo. Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, ila hunichukia mimi, kwa sababu mimi huushuhudia ya kwamba kazi zake ni mbovu. Ninyi nendeni katika sikukuu hiyo. Mimi siendi sasa katika siku kuu, maana saa yangu haijafika. Alipokwisha kuwaambia maneno haya, alizidi kukaa huko Galilaya zaidi.” Ndugu zake walisema naye kama watu wenye mamlaka. Aliyakanusha maneno yao, akiwahesabu kuwa sio wafuasi wake, ila ni watu wa ulimwengu tu. Ulimwengu hauwezi kuwachukia, kwa sababu wanafanana nao, ila huwapenda kama wenzao.TVV 255.1

    Yesu hakupaswa kuwa mwenye kiburi, wala hakujitia hatarini, ovyo, ovyo au kuharakisha matatizo yamjie. Alijua kuwa atachukiwa na ulimwengu, na kazi yake itaishia katika mauti, lakini kuharakisha na kujitia hatarini bila sababu, siyo mapenzi ya Mungu, ambaye ni Baba.TVV 255.2

    Watu wengi walikuja katika sikukuu kutoka pande zote, wakiwa na kusudi la kumwona Yesu. Mafarisayo na wakuu walimtazamia na kumtafuta wakitumaini kuwa wakati umefika wa kumshitaki. Waliuliza kwa makini wakisema: “Yuko wapi?” Lakini hakuna mtu aliyejua mahali alipo. Hakuna mtu aliyethubutu kumtaja kuwa Masihi, lakini kila mahali watu walikuwa wakiongea habari zake. Wengi waliamini kuwa alitumwa kutoka mbinguni kwa Mungu, wakati wengine wakimwita kuwa ni mdanganyifu.TVV 255.3

    Wakati ule ule Yesu alifika Yerusalemu kwa ghafla. Kama angalifuatana na msafara wa watu angejulikana na watu, na hoihoi kwa ajili yake zingezidi, na chuki ya wakuu ingechochewa juu yake.TVV 255.4

    Katikati ya sikukuu, Yesu aliingia hekaluni katika mkutano. Ilisemekana kwamba hawezi kujiingiza mwenyewe katika hatari ya makuhani na wakuu wa Kiyahudi wanaomchukia. Watu wote walistaajabia kutokea kwake wakati huu. Watu wakanyamaza kimya.TVV 255.5

    Akasimama katikati huku akitazamwa na watu wote, aliwahutubia kwa namna ambayo mtu hajafanya hivyo. Maneno yake yalionyesha ujuzi kamili wa kujitoa na kufanya huduma ya kicho hasa, akafundisha mafundisho ya manabii, kuliko makuhani na marabi wanavyofundisha. Alinena kwa uwezo kama mtu aonaye mambo yasiyoonekana na alisema kama mtu mwenye mamlaka ya mbinguni na duniani. Watu walishangaa kwa mafundisho yake, kama watu wa Kapernaumu walivyoshangaa, maana maneno yake “yalikuwa na uwezo”. Luka 4:32. Alifanya kila jambo liwaelekeze kutubu. Asingalikataliwa na watu wake, kama anawaokoa kutoka katika hatia ya dhambi.TVV 256.1

    Wakaulizana, ‘Mtu huyu amepataje kujua mambo, naye hajajifunza katika shule?” Yesu na Yohana Mbatizaji wamekuwa wajumbe wa kweli kabisa, na hali hawakujifunza shuleni, mwa Marabi, ambao ndio wakufunzi maalumu. Watu waliowasikia walishangazwa kwa jinsi ujuzi wao wa maandiko ulivyo. Lakini Mungu wa mbinguni ndiye aliyewafundisha. Yesu alipohubiri hekaluni watu waliachama tu. Waliokuwa wakimchukia sana, hawakuwa na jambo la kusema, wala kutenda.TVV 256.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents