Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    81 — “Bwana Amefufuka”

    Usiku wa siku ya kwanza ulikuwa umepita pole pole. Kristo alikuwa bado mfungwa katika gereza la kaburi lake. Muhuri wa Kirumi ulikuwako kwenye jiwe la kaburini; na askari wa Kirumi wakiwa katika zamu yao ya kulinda kaburi. Kama ingewezekana mkuu wa giza angeendelea milele kumfungia Mwana wa Mungu kaburini. Lakini malaika wa mbinguni wenye uwezo mwingi zaidi walikuwa wanasubiri kumkaribisha Mkuu wa uzima.TVV 441.1

    “Na tazama palikuwa na tetemeko kubwa la nchi, kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni.” Nuru kuu ya utukufu wa Mungu iliangaza njia yake. “Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji.” Na kwa kumwogopa wale walinzi, wakatetemeka wakawa kama wafu.”TVV 441.2

    Mjumbe huyu ndiye aliyechukua cheo Shetani alichokuwa nacho mbinguni kabla hajaasi. Alipokuwa akiliviringisha lile jiwe lililowekwa kaburini, mbingu ilionekana kana kwamba inashuka chini. Askari walimwona akiliondoa jiwe lile kubwa kana kwamba anaondoa kijiwe cha changarawe, na wakamsikia akinguruma na kusema; “Mwana wa Mungu, toka uje; Baba yako anakuita.” Walimwona Yesu akitoka kaburini, na wakasikia akitangaza juu ya kaburi lililopasuka, “Mimi ndimi huo ufufuo na uzima.” Alipotoka kwa fahari na utukufu jeshi la malaika likamlaki kwa nyimbo za shangwe.TVV 441.3

    Walinzi wa Kirumi walipowaona wale malaika na Yesu mwenye utukufu walizimia wakawa kama wafu. Wakati msururu wa utukufu ulipokwisha kutoweka machoni pao ndipo askari waliamka na kuondoka hali wakipepesuka kama walevi, kwenda mjini, wakiwaeleza watu waliokutana nao habari za ajabu zilizowatokea. Walikuwa wanaelekea kwa Pilato, lakini makuhani na wakuu wakawaita kwanza waletwe kwao. Askari wakiwa wanatetemeka na kutweta waliwaeleza mambo yote waliyona yalivyotokea. Askari walisema: “Hakika aliyesulibishwa alikuwa Mwana wa Mungu, tulisi-kia malaika akimtaja kwamba ni Mtukufu wa mbinguni, Mfalme wa utukufu.TVV 441.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents